Na Joseph Ngilisho Arusha
MAHAKAMA kuu Masijala Kuu kanda ya Dar es salaam imepanga Novemba 15 mwaka huu kutaja tarehe ya kuanza kusikilizwa kwa shauri la kupinga kipengere cha umri wa chini kwa mtoto wa kike kuolewa kuwa ni miaka 15.
Akiongea na vyombo vya habari jijini Arusha,mleta maombi katika shauri hilo,Mary Mushi kutoka shirika la kusaidia Ustawi wa wanawake na watoto (Women and Children Welfare Support).
Alisema kuwa shauri hilo namba 14 la mwaka 2022 lilifunguliwa dhidi ya wakili mkuu wa serikali kupinga mchakato wa kukusanya maoni kuhusu maboresho ya sheria ya ndoa .
Alisema mahakama hiyo mbele ya jaji Mosses Mzuna imetoa siku mbili kwa waleta maombi kwa ajili ya kuwasilisha maombi ya nyongeza na tarehe 15 Novemba mwaka huu, shauri hilo litatajwa tena kwa ajili ya kupanga siku ya kusikilizwa .
Alisema katika shauri hilo wanapinga maboresho ya sheria ya ndoa iliyotangazwa na waziri wa sheria na katiba ,dkt Damas Ndumbaro kuhusu kipengere cha umru wa chini kwa mtoto wa kike kuolewa kuwa chini ya miaka 15.
Katika mahakama hiyo waleta maombi wanaiomba mahakama itoe tamko kwamba umri wa chini wa kuolewa kwa mtoto wa kike ni miaka 18.
Pia wanaiomba mahakama itoe amri ya kusimamisha mahusiano yanayoendelea kuhusu umri wa chini ya mtoto wa kike kuolewa kwa sababu yanadhoofisha jukumu ,nafsi na hadhi ya mahakama ya Tanzania.
Alisema mahakama hiyo itamke kuwa kuanzia juni 7,2017 kifungu cha 13 na 17 cha sheria ya ndoa kilikoma kuwa sehemu ya sheria ya Tanzania.
Waziri wa Sheria na Katiba ana wajibu wa kikatiba wa kuheshimu na kutekeleza maamuzi ya mwisho yaliyitolewa ha mahakama ya Tanzanua bila icheleweshaji usio stahili
Ends...
0 Comments