FRIEND'S OF BATULI FUNGA KAZI ,YAMWAGA MISAADA YA KUFA MTU ,YAKABILI MAISHA YA WATOTO YATIMA ARUSHA

Na Joseph Ngilisho Arusha 

KIKUNDI cha kijamii cha Friends of Batuli cha jijini Arusha kimetoa msaada wa vyakula mbalimbali ,sabuni,mafuta na masweta kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha KIBOWA baada ya kubaini kwamba watoto hao wanahali ngumu ya maisha .

Kiongozi wa kundi hilo ,Batuli Kisaya alisema alipata maombi ya kutembelea kituo cha KIBOWA kilichopo mtaa wa Olopolosi,kata ya Terat, pembezoni mwa jiji la Arusha na baada ya kufika alitokwa machozi kujionea maisha magumu ya watoto hao zaidi ya 20 wanaolelewa kituoni hapo.


Alisema alitoka na kwenda kushauriana na wanakikundi wenzake ambao bila hiyana walikubaliana kuchangishana  na kupata msaada huo ,ambao ukitumika vizuri utawasidia kwa muda wa miezi mitatu.


Kisaya alitoa rai kwa jamii kutambua malezi bora ya watoto na kujiweke kando na mifarakano isiyo na tija inayopelekea kutengana na watoto kukosa malezi ya baba na mama na hatimaye  kuongezeka kwa wimbi la watoto mtaani
Mmoja ya wanachama wa kundi hilo Nasibu Mkopi,alisema kuwa kikundi hicho kimekuwa na taratibu za kujitolea kusaidia makundi maalumu yasiyojiweza kupitia faida kidogo wanayopata kwenye kazi zao .

Alitoa wito kwa vikundi vingine kuona umuhimu wa kujitoa kusaidia makundi hayo maalumu kwani kwa kufanyahivyo kutasaidia  kupunguza wimbi la watoto kukaa mitaani .


Awali mkurugenzi wa kituo  hicho cha Kibowa,Sifael Mkramweni alisema kituo hicho kilianzishwa mwaka 2005 kikiwa na watoto nane na mpaka sasa kina jumla ya watoto 22 na watoto wengi wanaletwa kutoka ustawi wa jamii. 


Alisema changamoto kubwa  ya kituo hicho ni kukosa  wafadhili wala mradi wa kuendesha kituo hicho lakini anamshukuru mungu watoto hao hawakuwahi kulala na njaa na wanakwenda shule.

Alisema kituo hicho kilichopo umbali wa kilometa 17 kutoka mjini Arusha ,wanategemea zaidi wahisani kuendesha maisha ya watoto hao na wamewaomba wahisani wengine kuiga kundi cha friends of batuli ambao wamekuwa msaada mkubwa katika ustawi wa watoto hao.

Ends..
.






Post a Comment

0 Comments