Na Joseph Ngilisho Arusha
KUSIMAMISHWA kwa Uchaguzi wa wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC)Mkoa wa Arusha kumepokelewa kwa shangwe na wanachama wa chama hicho mkoani hapa wakidai kwamba vitendo vya rushwa vimekuwa tatizo kwa wagombea.
Tamko la kusimamishwa kwa uchaguzi huo uliokuwa ufanyike kesho(leo)limetolewa na Katibu mkuu wa ccm Taifa Daniel Chongolo wakati akiongea na vyombo vya habari jijini Dodoma.
Kada maarufu wa ccm mkoani hapa,Ally Jumanne alisema kuwa hatua ya katibu mkuu wa ccm Taifa kufuta uchaguzi huo ni jambo la kizalendo akidai mmoja ya mgombea wa nafasi hilo ambaye ni mfanyabiashara mkubwa alilazimika kutumia Helkopta kwenda wilayani kushawishi wajumbe kwa kuwamwagia fedha kitendo ambacho sio sahihi.
"Kuhusu katibu kufuta uchaguzi kwanza amechelewa sana chaguzi nyingi zilizofanyika rushwa ilitembea ila huu wa unec umezidi sana kwa rushwa sijui hawa Takukuru wako wapi hapa Arusha hii ni aibu sana kwa ccm"
Wagombea wanaowania nafasi hiyo ya UNEC Mkoa wa Arusha ni pamoja na Bilionea wa Madini ya Ruby ,Gabriel Sendeu Laizer na Mfanyabiashara maarufu Arusha,Genso Bajuta.
Wengine ni Judith Mollel ,Daniel Palangyo na mwandishi wa habari wa Channel ten,Novatus Makunga.
Mwanachama mwingine wa ccm , Saimoni Laizer alienda mbali zaidi alidai kuwa chama hicho kinapaswa kufuta kabisa uchaguzi huo na kuanza upya mchakato wa wagombea kwa sababu baadhi ya wagombea wamekosa uzalendo.
"Mimi ni mwanachama hai wa ccm na mjumbe kutoka Arumeru kitendo nilichokishuhudia kwa macho yangu hakifai kabisa kwani wajumbe walikuwa wakipatiwa sh, elfu 50 hadi laki moja na mmoja ya mgombea alikuwa akitembea kwa Helkopta kuwafuata wajumbe"alisema Laizer.
Taarifa zimedai kuwa siku ya uchaguzi wa UWT Mkoa wa Arusha uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano AICC mwishoni mwa wiki ,mgombea mmoja mzito alionekana akirandaranda eneo la uchaguzi amiwasaka baadhi ya wajumbe na kuwakabidhi kitita cha noti kupitia wapambe wake waliokuwa wakigawa vipeperushi na fedha kama njugu.
Baadhi ya wanaccm walihoji udhaifu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru mkoani wakidai imelala usingizi wa pono na kushindwa kusimamia majukumu yao wakati fedha zilikuwa zikigawiwa hadharani.
Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha ,Musa Matoroka alipohojiwa juu ya hatua ya katibu mkuu taifa kusimamisha uchaguzi huo katika mkoa wake alidai kuwa taarifa hivyo ameipokea na yeye hawezi kuzungumza chochote kwa sababu ni tamko kutoka kwa viongozi wake wa ngazi za juu.
"Ni kweli taarifa nimeipokea kupitia vyombo vya habari wakati katibu mkuu akiongea sisi hapa Arusha hatuwezi kuongea chochote ispokuwa tunapokea maelekezo"
Matoroka ambaye hakuonesha kukiri ama kukataa vitendo vya rushwa mkoani kwake alisema kuwa katibu mkuu taifa ameona umuhimu wa kusimamisha uchaguzi huo kupitia macho yake yaliyopo mkoani hapa.
Gazeti hili lilimtafuta mmoja ya wagombea wa nafasi hiyo, Gesso
Bajuta,ili kupata maoni yake kuhusu tuhuma za rushwa kusimamisha uchaguzi kupisha uchunguzi,alidai kuwa amepokea taarifa hiyo ila alidai kuwa hakuwahi kukutana na wajumbe.
"Chama kimeamua kufuta uchaguzi wake na sisi kama wagombea hatuwezi kupingana na maamuzi hayo ,tunakubaliana nayo "alisema Bajuta
Kwa mujibu wa Chongolo , sababu kuu ya kufuta uchaguzi huo ni vitendo vya rushwa ambavyo vimetajwa katika maeneo hayo na kuwa chama hakitavulimia vitendo hivyo pale inapobainika ikiwemo kufuta kabisa uchaguzi huo.
Ends......
0 Comments