Na Joseph Ngilisho Arusha
WATU watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi akiwemo mwanamke mmoja ,wanashikiliwa na polisi mkoani hapa mara baada ya kunusurika kifo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali baada ya kukurupushwa wakitekeleza jaribio ya uporaji katika kanisa Katoliki la sant .Thereza lililopo jirani na kituo cha polisi jijini Arusha.
Watu hao wanadaiwa kutekeleza tukio hilo majira ya saa saba mchana baada ya kulifuatilia gari la Padri anayedaiwa kutoka benki na kuingia katika kanisa hilo .
Watu hao wanadaiwa kutumia gari ndogo yenye namba T 172 DTK ambalo hata hivyo lilishambuliwa na kuvunjwa kioo cha mbele na wananchi wenye hasira kali baada ya kufanikiwa kuidhibiti gari hiyo likiwa ndani ya uzio wa kanisa na baadaye polisi kufika .
0 Comments