UTEUZI :TAZAMA JINA LAKO HAPA ...KAMA HALIPO UJUE HUJATEULIWA


BY NGILISHO TV Dar es Salaam. 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imewateua madiwani 10 wa viti maalum kujaza nafasi zilizoachwa wazi katika halmashauri 10 za Tanzania Bara ambao wote ni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Taarifa iliyotolewa leo Jumapili Oktoba 30, 2022 na NEC imeeleza uteuzi huo umefanyika baada ya tume hiyo kupokea barua kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), ikielezea uwepo wa nafasi za wazi za madiwani wanawake.


Madiwani walioteuliwa wote ni wa CCM ambao ni Lidia Msongole wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya, Mariam Makasi (Mpwapwa), Bahati Shaban (Nzega), Sauda Irumba (Kaliua), Theresia Mlay (Moshi).

Wengine ni Monica Madiwa halmashauri ya wilaya ya Handeni, Hadija Ngope (Monduli), Hapines Kingu (Iramba), Zainab Mabrouck (Kongwa) na Zanaibu Orty wa Jiji la Dar es Salaam.


Katika hatua nyingine, NEC imesema uchaguzi wa mdogo wa jimbo la Amani,  Zanzibar na kata 12 za Tanzania Bara utafanyika Disemba 17 mwaka huu. Imesema Novemba 24 hadi 30 mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu.


“Novemba 30 uteuzi wa wagombea, Disemba Mosi hadi 16 kampeni na Disemba 17 siku ya kupiga kura,” imeeleza taarifa hiyo.


Kwa mujibu wa NEC, kata zitakazofanywa uchaguzi huo ni Majohe (Dar es Salaam), Dabalo (Dodoma), Ibanda (Mbeya), Mndumbwe (Mtwara), Njombe Mjini (Njombe), Misugusugu na Dunda (Pwani),Kalumbeleza (Rukwa), Mwamalili (Shinyanga), Mnyanjani, Lukozi, Vibaoni (Tanga).

Post a Comment

0 Comments