TRA ARUSHA YATAMBA KUVUKA LENGO LA MAKUSANYO YA KODI

 


Na Joseph Ngilisho Arusha 

MAMLAKA ya Mapato Tanzania TRA,mkoa wa Arusha imevuka lengo la makusanyo ya kodi ya sh,bilioni 390.5 iliyojiwekea katika kipindi cha mwezi julai 2021 hadi juni 2022 na kufikia kiasi cha sh,bilioni 411.7 sawa na asilimia 105.

Akiongea katika hafla fupi ya wiki ya huduma kwa mteja iliyofanyika katika ofisi za mamlaka hiyo,meneja wa TRA mkoani hapa,Eva Raphael alisema kuwa lengo la makusanyo katika kipindi hicho walijiwekea kukusanya kiasi cha sh,bilioni 390.5 lakini ushirikiano mzuri na walipa kodi umepelekea kuvuka lengo.

"Kutokana na ulipaji wenu mzuri wa kodi tumeweza kufanikiwa kukusanya kiasi cha sh,bilioni 411.7 sawa na asilimia 105 na hivyo kuvuka lengo tuliojiwekea"
Aliwataka walipa kodi kuendelea kushirikiana na mamlaka hiyo ili  kutatua changamoto zilizopo na kuimarisha  mahusiano .

Meneja aliahidi kuendelea kutoa elimu ya mlipa kodi na kutoa huduma kwa kufuata mkataba wa huduma kwa mteja ,haki zake na wajibu wake.

Aliwashukuru wateja kwa mchango wao mkubwa wanaoutoa kwa mamlaka hiyo kwa mwaka wa fedha uliopita uliofanikisha TRA kuvuka malengo ya nakusanyo waliojiwekea.

"Niwaombe wateja wetu muendelee kulipa kodi kwa hiyari ili nchi yetu iweze kufikia malengo yake na kutekeleza miradi mikubwa kwa maendeleo ya Taifa letu"

Mmoja ya wateja wa TRA ,Mwedi Mbaraka aliipongeza mamlaka hiyo kwa kujenga mahusiano mazuri na mlipa kodi jambo ambalo limesaidia kwa walipa kodi kutambua wajibu wao.


Aidha aliishauri TRA kuboresha huduma zake kwa kuongeza idadi ya watoa huduma ili kuondoa msongamano ya watu kucheleweshewa huduma .

"Zamani kulikuwa na changamoto nyingi ikiwemo wateja kufungiwa biashara zao sababu ya  kukwepa kodi kwa sababu hawakuwa na elimu ya mlipa kodi ila kwa sasa mambo mengi yameboreshwa na watu wanajitambua ndio maana mnavuka malengo"

Ends...



Post a Comment

0 Comments