Na Joseph Ngilisho, ARUMERU.
WAZAZI wametakiwa kuacha tabia ya kuwaficha watoto wao wenye ulemavu kwa madai ya kukwepa aibu badala yake wawapeleke shule ili kuwajengea uwezo wa kumudu maisha yao ya baadaye.
Aidha wazazi na walezi wanaoishi karibu na shule zinazowazunguka wameaswa kuzitumia shule hizo kuwapeleke watoto wao ili kuepuka gharama zinazotokana na usafiri.
"Natoa wito kwa wazazi wenye watoto wenye matatizo ya ulemavu wa aina yoyote ile kuachana na dhana ya kuwaficha majumbani watoto hao, badala yake wawapeleke shule ili wapate elimu kama walivyowatoto wengine na watumie fursa ya shule zilizoko kwenye mazingira yetu"Awali mkurugenzi wa shule hiyo,Bonface Mollel alisema kuwa shule yake ilianzishwa mwaka 2009 kwa lengo la kutoa elimu jumuishi kwa watoto wenye ulemavu na wakawaida ambapo kwa sasa watoto wapatao 38 wenye ulemavu wa viungo wanasomeshwa bure.
Mollel alisema kuwa shule hiyo ambayo ipo kwenye makazi ya jamii imekuwa mkombozi mkubwa kwa kusaidia jamii ya wafugaji kuwaibua watoto wenye ulemavu ili kuwapatia elimu bure na wengine kuchangia gharama ndogo.
Aliwataka wazazi kutowanyanyapaa na kuwaficha watoto wenye ulemavu ila wawafichue na kuwaleta katika shule hiyo ili wapate elimu iliyobora itakayowasaidia baadaye kwenye maisha yao
"Kabla shule hii hatujajenga wazazi wa kimasai walikuwa wagumu sana kuwatoa hadharani watoto wao wenye ulemavu lakini baada ya kuwapatia elimu naona wengi wamebadilika na wanawaleta hapa shuleni"
Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo ,Salimu Mlavi alisema jumla ya wamafunzi wapatao 20 wamehitimu masomo yao ya darasa la saba na kutunukiwa vyeti .
Aliwaasa wanafunzi hao kutoridhika na kiwango cha elimu walichofikia kwani huo ni mwanzo tu wa maisha ya kitaaluma.
0 Comments