TAZAMA RC MONGELA ALIVYOSHUHUDIA MABILIONI YA TOZO YAKIMWAGIKA ARUSHA

 

Na Joseph Ngilisho Arusha 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amewataka wakandarasi 18 waliosaini mikataba  ya kutengeneza miundo mbinu ya barabara na madaraja mkoani hapa, kufanya kazi kwa weledi na  uzalendo kwa kuzingatia muda na wale watakaoenda kinyume ametishia kuwafutia kufanyakazi katika mkoa huo.

Mongela ameyasema hayo jana wakati alipokuwa akishuhudia utiaji saini wa mikataba 18 yenye thamani ya sh,bilioni 4 kati ya Wakala wa barabara vijijini na Mijini ( TARURA) na wakandarasi 18 ,ikiwa ni fedha za nyongeza zilizotokana na tozo.
Katika hatua hiyo Mongella aliwataka wakandarasi hao kufanyakazi kwa  kufuata miongozo iliyopo kwenye mikataba yao , kwa kutekeleza mradi kwa viwango na kuepuka ubabaishaji, ucheleweshaji na kutokidhi ubora wa mradi.


Alisema, kukamilisha kwa barabara hizo kwa wakati na kwa viwango kutasaidia kushusha gharama za maisha kwa wananchi.

Aidha, amewaelekeza TARURA wakawasimamie wakandarasi hao kwa ukaribu zaidi ili wakamilishe miradi hiyo kwa wakati.
Meneja wa TARURA Mkoa wa Arusha mhandisi  Laynas Sanya alisema kwa mwaka wa fedha 2022/2023 walipatiwa jumla ya fedha za matengenezo ya barabara  zaidi ya  bilioni 18 kwa awamu ya pili na katika awamu ya kwanza mikataba 34 ilisainiwa yenye  thamani ya bilioni 14.
Alisema  awamu ya pili ya utiaji saini  jumla ya mikataba 18 yenye thamani ya zaidi ya sh,bilioni 4.071,921,007.26 imesainiwa na wakandarasi mbalimbali wazawa watakaotekelez miradi ya miezi sita kwa kiwando na ubora wa hali ya juu.

"Mikataba hii tumesaini ikiwa ni kufuata mwongozo wa rais Samia suluhu ambaye alielekeza mikataba yote isainiwe hadharani bila kusiri wowote"
Alisema wakati wa utekelezaji wa miradi ya barabara mwongozo wa serikali unawataka pia kuweka taa za  barabarani jambo ambalo alisisitiza  wameanza kulitekeleza.

"Mikataba iliyosainiwa leo ni kutengeneza barabara kwa kiwango cha Lami,ujenzi wa makaravati,ujenzi wa madaraja ya mawe ,ujenzi wa mifereji na matengenezo ya kawaida ya barabara"
Hata hivyo alisisitiza kuwa Tarura itahakikisha inawasimamia wakandarasi hao kuhakikisha miradi hiyo inatengenezwa kwa kiwango cha juu na kukamilika kwa wakati ndani ya miezi sita.

Naye, Mmoja ya wakandarasi Rashidi Sevingi  kutoka kampuni ya Raly (EA) Limited aliishukuru serikali kwa kuwaamini na kuwapatia kandarasi hizo kwani hapo awali walizoea kuona kandarasi nyingi zinakwenda kwa makapuni ya kigeni.
Aliwasihi wakandarasi wenzake  kutekeleza mikataba waliyosaini kwa weledi ili waendelee kuaminiwa zaidi na Serikali .

Ends..

Post a Comment

0 Comments