Na Joseph Ngilisho Arusha
NAIBU waziri wa fedha ,Hamad Chande amewataka watanzania kutumia fursa ya bima ya kimataifa ya mtu wa tatu (Yellow Card) kama njia moja wapo ya kukuza biashara na uchumi wa nchi na kuwarahisishia wafanyabiashara wanaosafiri kibiashara nje ya nchi.
Chande ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa 36 wa baraza la usimamizi wa bima ya mtu wa tatu NIC, unaokutanisha wanachama wa Soko la pamoja la Mashariki na kusini mwa afrika (COMESA) na wasiowanachama ,unaofanyika kwa siku tatu jijini Arusha.
Aliwataka wananchi na wafanyabiashara kutumia yellow kadi halisi na sio feki kama ilivyo kwa baadhi ya watu ambao wamekuwa wakihujumu taifa kwa kufumia kadi zisizosahihi.
Alifafanua kuwa faida ya yellow kadi unaweza kuitumia popote katika nchi yoyote wanachama ili kukinga biashara au ajali ukiwa nje ya nchi.
"Unapokata kadi ya Njano Tanzania unaweza kutumia kadi ile ile nchi za jirani kwa thamani ile ile ulionunua katika nchi husika na hii ni faida kubwa kibiashara kwa wafanyabiashara wanaochukua ama kupeleka bidhaa nje ya nchi"
Alisisitiza kuwa unapokuwa na kadi ya njano ni kinga kwa biashara hasa pale kunapotokea dharura ya ajali ya gari au ya moto katika biashara kunakufanya usisononoke kwa kuwa bima hiyo itakulipa fidia mali zako.
Aliitaka baraza la msimamizi wa bima ya mtu wa tatu (yellow kadi)kulipa fidia kwa waathirika wakati ndani ya simu 30 ili mtu awe na imani na mashirika ya bima.
Awali mkurugenzi mtendaji shirika la bima nchini NIC dkt Rehema Dorie alisema kuwa mkutano huo unakutanisha nchi wanachama wa soko la pamoja la mashariki na kusini mwa afrika (COMESA) na wasio wanachama zinazofanyabiashara ya bima ya mtu wa tatu.
Dkt Dolie ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la usimamizi wa bima ya mtu wa tatu kwa nchi za COMESA alisema yellow kadi inampa kinga na kumrahisishia mfanyabiashara anayesafiri ama kusafirisha mizigo katika nchi za comesa bila hofu ukizingatia kwamba Tanzania ni kitovu cha biashara kwa kuwa inabandari kubwa zinazopokea mizigo .
"Mtu akikata bima ya kadi ya ⁸Njano ya mtu wa tatu inaruhusu kuweza kupita na gari katika nchi zilizotuzunguka ikiwemo Zambia Malawi, Zimbabwe, Uganda Rwanda ,Burundi ,Msumbiji ,Jibuti na Sudani kusini na Sudan bila kusimamishwa na iwapo atasababisha madhara yoyote kwa mtu wa tatu bima hii inalipa mara moja kutokana na sheria za nchi husika bila kujali gharama zilizopo".
"Kadi ya Njano tayari ni jukwaa la ubadilishaji wa mali kwa njia ya kidigiti linalokua kwa kasi zaidi na salama barani Afrika. ”
Ends....
0 Comments