KATIBU UVCCM AJERUHIWA VIBAYA NA MCHEPUKO WAKE AMBAYE MWENYEKITI UWT

Na NGILISHO  TV,DODOMA 


KATIBU wa {UVCCM} wa Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma,Ramadhani Kiula amejeruhiwa vibaya kichwani kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali na Mwenyekiti wa UWT ,Fatuma Ramadhani anayedaiwa ni mchepuko wake baada ya  kumfuma  na mchepuo mwingine aitwaye ,Hamida Kondo ambaye ni mmiliki wa mgahawa akilishwa chakula.

Habari kutoka eneo la tukio zilisema kuwa tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 10.30 jioni katika Mgahawa wa Mama Kondo ambao ni maarufu katika Mji wa Chemba na unamilikiwa na mfanyabiashara Hamida Kondo.
Vyanzo vya habari vilisema kuwa Katibu wa UVCCM alijeruhiwa vibaya kichwani kwa kupigwa na jagi la maji baada ya kukutwa na mmiliki wa Mgahawa huo anaye3daiwa ni mcheouko wake, wakiwa wamekaa pamoja wakilishana chakula .

Hata hivyo Mmiliki wa Mgahawa,Hamida Kondo alipoulizwa na gazeti hili juu ya tukio hilo na yeye kuhusishwa na sakata hilo alikiri kuwa ugomvi ulitokea na kusabaisha usumbufu mkubwa kwa wateja waliokuwa eneo hilo ila hakufafanua uhusiano wake na kiongozi huyo wa chama.
Hata hivyo Hamida Kondo alipoulizwa na gazeti hili juu ya tukio hilo na yeye kuhusishwa na sakata hilo alikiri kuwa ugomvi ulitokea na umechafua jina la mgahawa wake.

Kondo alisema kwa sasa mgahawa wake baadhi ya wateja wamesusa na kueleza kuwa mgahawa huo una wanawake wagomvi na kufanya biashara kuwa mbaya baada ya vurugu hizo.

Akizungumzia tukio hilo,Kondo alisema Katibu wa UVCCM alikuja muda huo kupata chakula na alihudumiwa na ilifika mahali yeye alienda kukaa naye kama mteja wake kwa upendo.


Kondo alisema ghafla alikuja Mwenyekiti wa UWT,Fatuma Ramadhani na aliomba maji ya kunawa ili aweze kula chakula anachokula Katibu na alipatiwa maji na wahudumu na alianza kula na kuanza kuhoji maswali kwa nini anakula chakula na Mume wake.

Alisema wakati wanakula Mwenyekiti wa UWT alikuwa akimhoji mmiliki wa Mgahawa kwa nini anatembea na Mume wake na Mmiliki huyo alisema kuwa yeye sio Mke wa Katibu kwani katibu Mke wake anamjua na yuko Jijini Dar es Salaam na familia yake

Kondo alisema Mke wa Katibu Kiula anamjua kwa kuwa alipokuja Mji Chemba alikuwa akija na familia katika mgahawa huo na kupata chai,chakula cha mchana na jioni na alimweleza Mwenyekiti wa UWT kuwa wao wote ni wezi hivyo haoni sababu ya kuoneana wivu.

 

Alisema baada ya kumweleza Mwenyekiti huyo wa UWT kauli hiyo ghafla alichukua jagi la maji na kumpiga nalo kichwani mara mbili hadi tatu Katibu wa UVCCM na alitokwa na damu nyingi na kukimbizwa hospital kwa matibabu zaidi.

Mwenyekiti wa UWT,Fatuma Ramadhani alipotafutwa na gazeti hili kuelezea mkasa huo alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kifupi kuwa hayo yameshapita tugange yajayo na hakuhitaji tena kulizungumzia suala hilo.

 Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma,Martin Otieno alipotafutwa na gazeti hili kuzungumzia tukio hilo alisema kuwa hakuwa na taarifa rasmi ila aliahidi kulifuatilia na kulitolea taarifa hapo baadae lakini alipopigiwa hakupokjea tena simu

Ends..

 

Post a Comment

0 Comments