Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi, limemuamuru Padri Sosthenes Bahati Soka (41) anayekabiliwa na mashtaka ya kubaka watoto watatu wa kike kuondoka katika nyumba za kanisa hilo.
Badala yake, barua ya Askofu wa Jimbo hilo, Ludovick Minde ya Septemba 26, mwaka huu ambayo gazeti hili limeona, amemweleza Padri huyo haruhusiwi kuishi katika nyumba za kanisa na atakuwa akiishi nyumbani kwa wazazi wake.
Hili linaweza kuwa pigo jingine kwa Padri huyo ambaye kwa sasa yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kesi zake, baada ya kanisa pia kumsimamisha kutoa huduma zote za kipadri katika kanisa hilo kubwa duniani.
Katika barua yake hiyo ambayo imesambaa mitandaoni, Askofu Minde alisema uamuzi huo umezingatia sheria ya kanisa namba 1,722 inayotaka mtuhumiwa kutengwa katika kipindi cha mchakato wa kisheria wa tuhuma zinazomkabili.
Sheria hiyo inasema ili kuzuia kashfa, kulinda uhuru wa mashahidi na kulinda njia ya haki, watu wa kawaida, baada ya kumsikiliza mtetezi wa haki na kumtaja mtuhumiwa, katika hatua yoyote ya mchakato inaweza kuwatenga mtuhumiwa na kazi za kikanisa.
Pia, sheria hiyo inasema kanisa linaweza kuweka au kumkataza kuishi mahali fulani au eneo fulani au hata inaweza kukataza ushiriki wa umma katika Ekaristi Takatifu zaidi na mara tu tuhuma zinapokoma na hatua hizi zote lazima zifutwe na pia huisha na sheria yenyewe pale mchakato wa adhabu unapokoma.
“Kwa masikitiko makubwa, kwa barua hii kuanzia leo tarehe 26/09/2022 umesimamishwa kutoa huduma zote za kipadri katika Kanisa Katoliki, pia huruhusiwi kuishi katika nyumba za kanisa. Utakuwa unaishi nyumbani kwa wazazi wako,”
alisisitiza Askofu Minde katika barua hiyo na kuongeza:
0 Comments