Na Joseph Ngilisho Arusha
Mkuu wa wilaya ya Arusha, Said Mtanda amewataka wadau wa elimu,wazazi na wanafunzi kujiandaa na mabadiliko ya mitaala na sera ya elimu ambayo imelenga kuboresha muundo wa elimu hapa nchini ili uendane na wakati.
Akiongea jana katika mahafali ya 12 ya wahitimu 73 wa shule ya sekondari ya Notredame
iliyopo Njiro jijini Arusha,alisema kwa sasa serikali ipo kwenye mkakati wa maboresho ya sera ya elimu na mitaala yatakayozingatia mahitaji ya wakati.
" Serikali yenu ya rais Samia kwa sasa inafanya mapitio ya sera ya elimu ili kuimarisha zaidi elimu kwa hiyo siku sio nyingi mkiwa wadau wa elimu mtayaona mabadiliko hayo ikiwemo elimu ya awali hadi kidato cha sita kuwa ni elimu ya msingi "
Aliwataka wahitimu kutoridhika na elimu walioipata kwa sasa bali waione kama elimu ya msingi na uwe mwanzo wa wao kuendelea mbele zaidi na wazingatie mafunzo waliyoyapata ili yaweze kuwasaidia huko waendako.
Awali mkuu wa shule hiyo,Sister Mary Olive alisema, wanaishukuru serikali kwa kila hatua ambayo inalenga kuboresha sera ya elimu hapa nchini na wao kama wadau wa elimu wapo tayari kupokea mabadiliko hayo .
Alisema wao kama taasisi wataendelea kushirikiana na serikali katika kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu iliyobora.
"Sisi kama taasisi ya elimu tupo tauaribkupokea maelekezo yoyote ya serikali kuhusu mabadiliko ya mitaala na sera ya elimu"
Mkuu huyo wa shule aliwaasa wahitimu ambao ni wanafunzi wa kike pekee kuhakikisha wanazingatia maadili yote waliojifunza shuleni hapo na anaamini elimu na maadili waliyoyapata hawatajutia .
Kwa upande wa baadhi ya wahitimu Veronica Sawe na Anneth Kimberely waliishukuru shule hiyo kwa kuwapatia elimu na maadili bora na kuahidi kufanya vizuri katika mtihani ujao wa kidato cha nne.
"Nashukuru kwa elimu niliyoipata naamini ndoto yangu itatimia kwani masomo tuliyojifunza hapa yametusaidia kikuza elimu yangu na kutujenge kiroho ,nategemea tutaenda kupata ufaulu mzuri sana"
Ends....
0 Comments