DARAJA LAPOROMOKA NA KUUA 132 .


BY NGILISHO TV 

Watu 132 wamefariki dunia baada ya daraja linalotumiwa na waenda kwa miguu kuvunjika katika jimbo la magharibi la Gujarat nchini India.


Picha za video zinaonesha mamia ya watu waliotumbukia katika mto Macchu ulioko kwenye mji wa Morbi wakipiga kelele za kuomba msaada huku wengine wakining'inia kwenye kingo za daraja lililokuwa likizama mtoni.


Waziri wa nchi katika Wizara ya Kazi na Ajira kwenye jimbo hilo la Gujarat Brijesh Merja amearifu kuwa zaidi ya watu 80 wameokolewa, katika daraja hilo ambalo wakati likipasuka kulikuwa na kiasi cha watu 400.


Tukio hilo limetokea siku chache tu baada ya daraja hilo kufunguliwa tena, kufuatia ukarabati uliokuwa ukifanywa.


Daraja hilo lililojengwa toka enzi za ukoloni katika karne ya 19, wakati wa utawala Uingereza lina urefu wa mita 230 na ni maarufu kama kivutio cha utalii katika eneo hilo.


Mmoja ya watu aliyeshuhudia ajali hiyo anasema kulikuwa na watoto wengi katika daraja hilo la wenda kwa miguu, wakati lilipokatika.


Prateek Vasava ni mmoja ya waliokuwa katika daraja hilo anasema mara tu tukio hilo liliovyotokea alitumbukia ndani yam aji na kujiokoa kwa kuogelea mpaka katika ukingo wa mto huo.


Anasema aliona pia Watoto wengi wakitumbukia mtoni,lakini alishindwa kuwaokoa Pamoja naye, akihofia kuzama ama kusombwa na maji.


Picha za video zinaonesha mtafaruku na hamaki za watu wakijaribu kujiokoa baada ya kutumbukia mtoni na wengine kukwamba katika kingo za daraja hilo refu kwenda juu, wakati giza likiingia.


Juhudi za uokoaji zimefanyika usiku kucha. Bado chanzo cha kuvujika kwa ajali hiyo hazijafahamika, lakini mamlaka za Enei hilo zinasemamsongamano wa watu katika daraja hilo wakati huu wa msimu wa sikukukuu ya diwali inaweza pia kuwa sababu

Post a Comment

0 Comments