Na Joseph Ngilisho Arusha
Jumla ya wakimbiaji wapatao 6000 kutoka mikoa mbalimbali nchini,wanatarajia kukimbia katika mbio za marathon za NMB zitakazofanyika Jijini Dar es Salaam septemba 24 mwaka huu.
Akiongea na vyombo vya habari Jijini Arusha wakati wa mazoezi ya kujifua kwa baadhi ya wanariadha wa timu ya taifa mkoano hapa,Meneja wa NMB Tawi la Clock Tower Emmanuel Kishosha amesema mbio hizo zitaanzia Leaders Club na kuishia hapo hapo.
Amesema Lengo la mbio hizo ni kuchangia matibabu ya akinamama wanaosumbuliwa na ugonjwa wa fistula kupata matibabu ndio maana wamezipa kauli mbiu ya NMB Marathon ,Mwendo wa Upendo huku wakitarajia kukusanya kiasi cha sh, milion 600.
Amesema mbio hizo ni awamu ya pili ambapo mbio za mwaka jana walikusanya sh, milion 400 ikiwa ni malengo ya kukusanya sh,bilion moja na hivyo kutimiza malengo yao.
"Tunatarajia kuwa na wakimbiaji takribani 6000 na mbio hizo zitakuwa urefu wa kilometa 5,10 na 21 hivyo watanzania wenzetu tunaomba tujiunge pamoja tuweze kuwachangia matibabu ya akina mama wanaosumbuliwa na ugonjwa wa fistula "alisema Kishosha.
Awali wakiongea na mabalozi wa mbio hizo pamoja na wachezaji wa timu ya taifa ya riadha Failuna Abdi Matanga na Emmanuel Giniki wamesema watashiriki mbio hizo kwa km 21 na mungu akiwapa Afya watashinda mbio hizo.
"Sisi wanariadha kutoka kanda ya Kaskazini tupo tayari kuunga mkono jitihada za NMB naamini na wengine watajitokeza kukimbia kwani mazoezi ni afya na pia kufanikisha kuchangia akina mama wanaosumbuliwa na fistula"alisema Giniki
Wamewataka watanzania kujitokeza kushiriki na kuchangia mbio hizo ikiwa ni kuwapa faraja na furaha wakinamama wanaosumbuliwa na Ugonjwa wa fistula.
Ends...
0 Comments