VIJANA WANASWA KWEUPE WAKIWA NA VYETI FEKI KATIKA ZOEZI LA USAHILI JKT

BY NGILISHO TV,ARUSHA.

Watu wawili Hamis  Makaranga na Godbless Lukumay wote wakazi wa Jiji la  Arusha wamekamatwa na jeshi la polisi mkoani hapa wakituhumiwa kutengeneza vyeti feki vya kuzaliwa ili kufanikisha zoezi la usahili nafasi za Jeshi la kujenga Taifa (JKT) linaloendelea ofisi ya mkuu wa wilaya ya Arusha.


Vijana hao walitiliwa shaka na kamati ya ulinzi na usalama iliyokuwa ikiendesha zoezi Hilo na ndipo ilipoamua kufanya uchunguzi na kugundua kuwa vyeti vyao vya kuzaliwa havikuwa sahihi .


Mkuu wa wilaya ya Arusha Said Mtanda ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama alisema kuwa Vijana hao walifilishwa kituo cha polisi na kuhojiwa na ndipo walipotaja mahala walipovipata.


"Nawapongeza wajumbe wa kamati ya usalama ya wilaya na jeshi la polisi wilaya ya Arusha kwa kufanikisha kukamatwa kwa wahakifu hao"Alisema DC Mtanda.



Post a Comment

0 Comments