VIJANA 130 WAHITIMU MAFUNZO YA WANAGENZI ni wale waliowezeshwa na serikali kupitia SIDO


 Na Joseph Ngilisho Arusha 



SERIKALI kwa kushirikiana na Shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO)kupitia mradi wa wanagenzi , imewawezesha vijana wapatao 130 mkoani Arusha ,kupata mafunzo ya ujasiriamali kupitia viwanda vidogo ,ambayo yamesaidia kuwapatia ujuzi na uthubutu wa kujiajiri kupitia sekta hiyo.


Hayo yamebainishwa na Katibu tawala Rasilimali watu Mkoani hapa,David Lyamongi wakati akifunga mafunzo ya mwezi mmoja kwa vijana hao 130 waliohitimu mafunzo ya viwandani kutoka kwa wanagenzi  pamoja na kuwatunuku vyeti , iliyofanyika jijini Arusha.



Lyamongi ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongela,alitoa rai kwa wahitimu hao kuhakikisha wanatumia uzoefu walioupa kubuni na kwenda kuanzisha viwanda vidogo vitakavyowasaida kujiajiri na kupunguza janga la ajira hapa nchini. 


Katibu tawala huyo alilipongeza shirika la SIDO kwa kutekeleza vema mradi huo unaosimamiwa na serikali kupitia wizara ya  Elimu,Sayansi na Teknolojia na  kufadhiliwa na benki ya dunia ambapo alisema ,serikali inatambua changamoto za vijana.



Awali meneja wa SIDO mkoa wa Arusha,Jafary Donge aliishukuru serikali kwa kukubali kuwapatia mafunzo na mitaji vijana hao ambayo yamesaidia kuwapa uzoefu mahala pa kazi.


Alisema hadi sasa mradi huo umefanyika katika mikoa 12 na kuwafikia vijana 1647nchini huku mkoa wa Arusha kupitia halmashauri ya Arusha DC,Meru na jiji la Arusha,ukiandikisha  vijana  130 wakiwemo wanawake 66 ambao wote wamehitimu na kupewa vyeti.

Alisema kuwa jukumu la SIDO  katika mradi huo ilikuwa ni kuratibu vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 35 ambao waliwahi kushiriki mafunzo kutoka SIDO na katika taasisi na vyuo mbalimbali.


"Baada ya kuwapata vijana hao tuliwaunganisha na wanagenzi ambao waliwapatia mafunzo katika viwanda vyao kwa muda wa mwezi mmoja huku serikali ikiwapatia kiasi cha sh.100,000 kila wiki kama fedha ya kujikimu "alisema.
Alisema vijana hao  walishiriki na kufuzu  mafunzo ya uokoji wa mikate,usindikaji wa vyakula,asali na Vipodozi,Utengenezaji wa Sabuni,Ushonaji,Uhandisi, ufundi magari , utalii na Urembo.


Baadhi ya wanagenzi,Ally Babu kutoka kampuni ya uokaji mikate ya Bilsarm ,Irene Baker na Ahmed Abdalah (Dallerz Group)waliipongeza serikali kwa hatua ya kuwapatia mafunzo vijana kupitia viwanda ikiwa ni njia mojawapo ya kukabiliana na wimbi la ajira hapa nchini. 

"Mpango huu ni mzuri kwani unatusaidia hata sisi kupata wafanyakazi bora tuliowafundisha wenyewe na pia utasaidia kupunguza wimbi la ajira kwa baadhi yao watakaojiajiri "alisema Irene Manzi anayemiliki  Irene Baker  eneo la Majengo na Maromboso jijini hapa.


Ends...










Post a Comment

0 Comments