Na Joseph Ngilisho, Arusha
BINTI wenye umri wa miaka 15,Mesoni Kashiro Mkazi wa Kijiji Cha Gelailumbwa kata ya Gelailumbwa Tarafa ya Ketumbeine wilayani Longido Mkoa wa Arusha amejeruhiwa vibaya kwa kipigo baada ya kushambuliwa na Mume wake akiwa amefungwa kamba kwenye mti na kuning'inizwa.
Mtuhumiwa aliyetajwa kwa jina la Namendea Lesiria alishiriki unyama huo akiwa na Rafiki yake ambaye jina lake halikufahamika mara moja kwa kumsgamvukia mke wake,wakimtuhumu kumwaga dawa ya mfugo.
Hayo yamebainishwa na Ofisa Ustawi wa Jamii wilayani hapa ,Atunagile Chisunga akieleza kuwa watuhumiwa wapo kituo Cha Polisi Longido na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani.
''Lakini Mama huyo Yupo kituo Cha afya Longido Kwa matibabau zaidi baada ya kujeruhuwa vibaya kwa kipigo''.alisema.
1 Comments
Hakuna mwanamke wa miaka 15 huyu ni mtoto, pia kuonyesha sura yake ni kuongeza ukatili
ReplyDelete