Mwenyekiti Mpya wa umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi UVCCM,wilaya ya Arusha, Hasan Mndeme ameahidi kuleta Mapinduzi makubwa kwa vijana katika nyanja za kiuchumi na kielimu.
Akiongea mara baada ya kuibuka mshindi kwa kupata kura 170 akifuatiwa na Issa Burhan aliyepata kura 89 huku Pauline Matei akiambulia kura 5 katika uchaguzi uliofanyika makao makuu ya chana hicho jijini hapa.
Mndeme aliwashukuru wajumbe kwa ushindi huo mkubwa na kuahidi kusimamia misingi sahihi ya chama, akishirikiana na viongozi na wanachama wa ccm.
Alisema uchaguzi huo ulikuwa na ushindani mkubwa ila hakuwa na mashaka na ushindi ,kwani alijipanga vizuri na aliwashukuru wapinzani wake kwa kukubali matokeo.
"Wake wanaosema nimepachikwa na kigogo fulani na sikuwa na uwezo wa kushinda wanakosea ,niliamua mwenyewe kuchukua fomu na kushikiri kunyang'anyiro hicho, nataka nifanyekazi niache alama maneno ya wanasiasa hayawezi kunivunja moyo"alisema
Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa amejipanga kuwapambania vijana kwa kuwajengea uwezo wa kiuchumi na kielimu .
Mndeme ambaye ni Mjasiriamali mdogo jijini hapa,alisema uchaguzi huo umemheshimisha na kuleta chachu kwa vijana akiwataka kutokata tamaa bali wawe na uthubutu.
"Vijana waache woga katika kujiingiza kwenye duru za siasa,ujasiriamali kwani hata yeye alithubutu na ndoto yake imetimia na aliahidi kufika mbali zaidi kisiasa.
Aliahidi kufanyakazi chini ya serikali ya rais Samia Suluhu ili kuwainua kiuchumi vijana wajivunie ufahari wa serikali yao na chama cha mapinduzi .
Ends...
0 Comments