TAZAMA, FAMILIA KATI KATI YA JIJI LA ARUSHA, YATOLEWA KIBABE NDANI YA NYUMBA YAO,YAMLILIA RAIS SAMIA KUWASAIDIA

 

Na Joseph Ngilisho ,Arusha 

Familia moja iliyopo mtaa wa Pangani ,kata ya mjini kati, jijini Arusha haina mahala pa kuishi baada ya kundi la watu kuvamia nyumba yao na kutupa nje vitu vyao vya ndani huku wakiwaacha wasijue la kufanya.

Tukio hilo limetokea jana majira ya mchana na kushudiwa na umati mkubwa wa watu waliokuwa wakipita eneo hilo wakati vijana hao wakitekeleza zoezi kwa kutupa nje vitanda, magodoro,vyombo  ,nguo na baadaye kuifunga nyumba hiyo kwa kufuri.
Akiongelea tukio hilo baba mwenye nyumba hiyo, Issa Okashi alibainisha kusikitishwa na kile alichodai ni unyama usio mithirika ,akidai tukio hilo limetendwa na dalali wa mahakama kutokana na kesi iliyokuwa mahakama ya mwanzo kati yake na  kaka yake aitwaye Said Okeshi ambaye kwa sasa ni marehemu.

Alisema uamuzi wa mahakama haukutendea haki kwani anaamini kwamba yeye ndiye msimamizi halali wa Mirathi ya marehemu na katika kipindi chote cha maisha yake amekuwa akiishi katika nyumba  hiyo .


Alifafanua kuwa awali kulikuwa na kesi katika Mahakama ya Mwanzo ya Maromboso,kesi iliyochukua takribani miaka 13 kumalizika na kaka yake aliyefungua kesi hiyo alifariki dunia mwaka jana kabla ya hukumu kutolewa.

Alisema mahakama ilitoa maamuzi ambayo hayakumridhisha  na aliamua kukata rufaa, lakini wakati anasikilizia kutajwa kwa kesi ya rufaa yake, ameshangaa kuona akiondolewa kibabe katika nyumba hiyo ,ambapo amemwomba rais Samia Suluhu  kuingilia kati ili  kumsaidia kuweza kupata haki yake ya msingi kwani anaamini kuna hila imetendeka.

Naye Mtoto wa Okashi ,Halima Issa alifafanua kuwa baba yake alizaliwa katika nyumba hiyo na amekuwa akiishi hapo katika kipindi chote cha maisha yake huku marehemu kaka yake ,Said Okashi akiwa jijini dar es salaam kwa muda mrefu
Alisema kuwa nyumba hiyo iliachwa na marehemu bibi yao, Mwajabu mbwana aliyefariki miaka kadhaa iliyopita na kuacha watoto wanne akiwemo baba yake , Issa Okashi. 

Alisema baba yake mkubwa,Said Okeshi aliamua kwenda mahakamani kufungua kesi akidai kuwa yeye ndio msimamizi wa Mirathi,akiiomba mahakama kumtambua , wakati hakuwahi kuishi katika nyumba hiyo wala kuchaguliwa na ndugu wa familia.

"Tumeshangaa leo kuvamiwa na dalali wa mahakama na kututoa nje ya nyumba wakidài ni amri ya mahakama na hii nyumba inatakiwa kuuzwa,hii sio sahihi kwani kesi bado ipo mahakamani"

Kwa upande wake dalali wa mahakama wa kambuni ya Nutmeg Auctioneers and Property Managers Co.Ltd,Bonface Buberwa anayetekeleza zoezi hilo,alisema kuwa kampuni yake ipo hapo kisheria na inatekeleza amri ya mahakama iliyotolewa tangu julai mwaka huu.

"Sisi tupo hapa kutekeleza amri ya mahakama iliyoamuru nyumba hii ibaki wazi ikiwa imefungwa na bila kuwepo mtu wala kitu chochote  ndani"alisema.

Mmoja ya ndugu wa familia hiyo,Abubakari Mlau aliitupia lawama mahakama kwa kutoa maamuzi ya kuwaondoa ndani ya nyumba wakati kuna kesi ya rufaa inayopaswa kusikilizwa  .

"Mimi nahisi mahakama haikutenda haki kwa upande wa Issa Okashi,  kushindwa kuzingatia kesi ya  rufaa aliyoifungua''

Ends....


Post a Comment

0 Comments