Na Joseph Ngilisho, ARUSHA
TAASISI mbalimbali za mazingira hapa nchini zimeanza mkakati wa kupambana na mimea vamizi aina ya Mrashia ambao unanyemelea ,bonde la ziwa Natron na kuathiri maeneo ya hifadhi za wanyapori na kilimo, kanda ya kaskazini.
Akiongea katika warsha ya Udhibiti wa mimea vamizi bonde la ziwa Natroni jijini Arusha,Afisa Mazingira Mkuu kutoka ofisi ya makamu wa Rais ,Fainahappy Kimambo alisema kuwa,ofisi ya rais kwa kushirikiana na wadau wameona tatizo la viumbe vamizi ni kubwa sana hapa nchini hivyo wameandaa mpango kazi wa usimamizi wa viumbe vamizi na unahitajika utekelezwe na wadau wote.
Amesema kuwa,mpango huo utatekelezwa kupitia wizara za kisekta, taasisi,na jamii kwa ujumla ambapo mkakati unasema kuwa kila sekta na mdau lazima aagize kwenye mipango yake wa kisekta na kwenye bajeti.
"Tatizo la viumbe vamizi ni kubwa sana kwa Tanzania na na hivyo mradi huo utasaidia kupambana na mmea vamizi aina ya Mrashia ambao umevamia sana maeneo ya ziwa Natron na kuzuia shughuli za kijamii ikiwemo ufugaji,kilimo na hivyo kusababidha jamii kutonufaika na rasilimali za ziwa Natron."amesema.
Amesema kuwa,ukiacha ziwa Natron maeneo mengine yaliyoadhiriwa na mmea vamizi ji pamoja na ziwa Jipe ,na ziwa Victoria na mabwawa mengine kama nyumba ya Mungu na maeneo ya malisho na kilimo yaliyopo eneo la Kahe na Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya jamii ya utafiti wa maendeleo (CoRDS),Lilian Looloitai amesema kuwa,wao ni watekelezaji wa mradi huo ambapo amesema swala la mimea vamizi ni janga la kitaifa hasa katika maeneo ya malisho na mazingira mengine ya kibinadamu.
Alisema kuwa,wao kama CORDS wameamua wawekeze nguvu kubwa katika kutatua na kungalia namna ya kukabiliana ba mmea vamizi kwa kushirikiana na jamii katika kuihamasisha ili kutambua mmea usio rafiki katika mazingira ya binadamu ili ichukue hatua kwa kuiondoa kabla haijaleta athari kubwa.
Alisema kuwa, mradi kama huo ni hitaji na wanaona ni changamoto kubwa kutokana ba mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo inasababisha uwepo wa mimea vamizi ,hivyo wanataka kuhakikisha kuwa wanaweka nguvu kubwa pamoja katika kutafuta rasilimali fedha na watu ili kukabiliana na mimea vamizi.
Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa misitu Tanzania TAFORI,Dkt Revokatus Mushumbusi alisema kuwa,utekelezaji wa mpango huo utashirikisha watafiti na wadau kutoka taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi.
Dk .Mushumbusi alisema kuwa,warsha hiyo imewakutanisha wadau kutoka taasisi za kiserikali, mashirika binafsi kutoka wilaya za Longido, Ngorongoro, Monduli na Karatu pamoja na wadau kutoka wizarani .
Naye Mkurugenzi wa jumuiko la maliasili Tanzania (TNRF),Zacharia Faustine ambaye ni mmbia mtekelezaji wa programmu ya kudhibiti mmea vamizi katika maeneo ya hifadhi ya Taifa na nyanda za malisho .
Alisema kuwa, lengo la taasisi hiyo ni kuhakikisha kuwa mimea vamizi ambayo inaingia kwa njia mbalimbali kutoka nje ya nchi wanaiondoa kwani imeathiri sana upatikanaji wa malisho kwa ajili ya wanyapori na mifugo.
Alisema kuwa, njia pekee ya kuidhibiti ni kuwaleta wadau pamoja wakiwemo Nemc na halmashauri za wilaya ili kuweza kujadili na kuja na njia mbadala ya kuweza kuiondoa mimea vamizi.
Ends...
0 Comments