SENSA IMEWEKA REKODI YA TANZANIA KIDUNIA:MTAKWIMU MKUU WA SERIKALI

Na Joseph Ngilisho, ARUSHA 

MTAKWIMU mkuu wa Sensa ya watu na makazi nchini ameipongeza taasisi ya dini ya kiislamu ya Twarika Qadiriya, viongozi wa mila na dini mkoani Arusha kwa kuipa heshina serikali kwa kufanikisha kuhamasisha wananchi kushiriki zoezi hilo na kuifanya  Tanzania kuingia kwenye rekodi ya kidunia.

Akisoma taarifa kwa niaba ya mtakwimu mkuu wa serikali,katika hafla ya kumpongez rais Samia Suluhu Hasan kwa kuandaa na kufanikisha zoezi hilo,Seif Kuchengo alisema kuwa taaisis hiyo ya dini ilikuwa mstari wa mbele katika kuratibu na kuyashirikisha makundi mbalimbali katika kuhamasisha zoezi la sensa hapa nchini.

Alisema kuwa ofisi ya mtakwimu  mkuu wa serikali haina budi kupongeza taasisi zote zilizoshiriki kufanikisha zoezi hilo ambalo ni sensa ya sita  hapa Tanzania.



Uhamasishaji uliofanywa na viongozi wa dini,wanasiasa ,viongozi wa wilaya na mkoa  hapa nchini umefanikisha Tanzania kuingia kwenye rekodi ya kidunia na kuwataka viongozi hao kuendelea na moyo huo wa kuunga mkoano kwenye masuala mengine ya maendeleo.

Alisema kwa kufanikisha zoezi hilo nchi yetu imekuwa miongozi mwa nchi za Afrika na dunia zilizofanya sensa ndani ya mzunguko wa miaka 2020 ,mzunguko ambao unazitaka nchi kufanya sensa ndani ya miaka 10 kuanzia mwaka 2015 hadi mwaka 2024.Hivyo Tanzania imeingia kwenye  rekodi hiyo.


Awali kiongozi wa Twarika mkoa wa Arusha,Sheikh Haruna Husein alimshukuru  rais Samia Suluhu hasani kwa kuandaa na kufanikisha zoezi la Sensa ya watu na makazi hapa nchini jambo ambalo litasaidia kuipa fursa serikali kuwaletea maendeleo  ya dhati wananchi wake.


Aidha sheikh Haruna pamoja na kuwashukuru viongozi wa dini mbalimbali makundi ya mama Ntilie,Bodaboda ,viongozi wa mila Laigwanan na washiri,wanasiasa na viongozi wa ngazi ya wilaya na mkoa alisema ipo haja ya kuendeleza mshikamano huo katika kuunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na umasikini.

Akiongea kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha,John Mongela, Leokadia Mtei ambaye ni mtakwimu mkuu mkoa wa Arusha, aliwashukuru wananchi wa mkoa wa Arusha kwa kufanikisha zoezi  hilo ambapo kwa Arusha wamefanikiwa kuandikisha watu na makazi kwa kiwango kikubwa na hivyo kuvuka malengo waliojiwekea.

Aliwataka wananchi kusubiri Takwimu halisi zitakazotolewa na serikali ambazo zitatangazwa na rais ili serikali iweze kupanga mikakati ya kuwaletea maendeleo yatakayowanufaisha wananchi .



Ends.










Post a Comment

0 Comments