WANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha mjini wamehoji Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ipo wapi wakati chaguzi ndani ya Chama hicho hususani Ngazi ya Jumuiya ya wazazi kugubikwa na vitendo vya rushwa za wazi wazi hadi vyooni.
Akizungumza mmoja wa wanachama wa chama hicho aliyekataa kutajwa jina hadharani alisema Taasisi hiyo imekuwa kimya bila kufuatilia matukio yanayoendelea ndani ya chaguzi za chama kutokea ngazi ya matawi kata hadi Wilaya ambapo kumekuwepo utoaji wa rushwa za waziwazi jambo ambalo sio mustakabali mzuri wa chama hicho.
Alisema zoezi la wagombea wenye majina makubwa wamekuwa wakitumia watu kugawa fedha na majiko ya magesi kwa wanachama ili kupanga safu za uongozi ndani ya chama hicho jambo ambalo siku za usoni litakuja kukigharimu chama hicho na kuhoji Taasisi hiyo jijini hapa,chini ya kamanda wake James Ruge, imekwama wapi kufuatilia masuala mazima ya rushwa ndani ya chama hicho kikomgwe.
Mwanachama huyo ameendelea kuwashukuru wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi kwa kuonyesha ukomavu na kuikataa rushwa iliyokuwa ikitembezwa ndani na nje ya ukumbi wa uchaguzi hadi ndanni ya vyoo wazi wazi hadi msimamizi wa uchaguzi huo ,Anna Msuya(M-NEC) baada ya uchaguzi wakati akishukuru na kufunga uchaguzi huo kutamka waziwazi kuwa kulikuwa na vitendo vya rushwa hadikuwatoa nje ya ukumbi wajumbe wawili akiwemo, Asia Mkali waliokuwa wanagawa rushwa ndani ya ukumbi huo hadi meza kuu.
Akiongea Mara Baada ya Uchaguzi huo Msimamizi wa uchaguzi huo Anna Msuya alisema uchaguzi huo umeonyesha mustakabali mwema na kuonyesha nguvu ya wanachama kukataa vitendo vya rushwa na kuonyesha ukomavu kutopangiwa wa kufuata maelekezo.
Akitangaza matokea hayo Msimamizi wa Uchaguzi huo Mjumbe wa Halmashauri kuu Anna Msuya Ally Mwinyimvua alipata kura 212 huku Meya Mstaafu Gaudence Lyimo akiambulia 61 na Bertha Laizer kura 1 hivyo kumtangaza Ally Mwinyimvua kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi kwa kipindi cha pili.
Hatahivyo Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Arusha James Ruge alipotafuta kwa njia ya simu alijibu kuwa hakuna tukio hilo kwani wanapopewa Taarifa huzifanyiakazi na kutaka mwandishi kutoa taarifa kabla ya kuuliza au kuhoji suala lolote kwa TAKUKURU mkoa.
"Nauliza ulileta taarifa kwetu hata uhoji tukio hilo kwetu suala la rushwa ni jukumu la wananchi wote hivyo kama ulitupa taarifa tueleze kwanza ndipo tujipo sasa hakuna tukio hilo" akijibu kwa kufoka
Ends...
0 Comments