RC ARUSHA AMTWISHA ZIGO RPC ARUSHA VISHKWAMBI VYA SENSA VILIVYOPOTEA

Na Joseph Ngilisho Arusha 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela ameliagiza jeshi la polisi mkoani hapa, kupitia mkuu wa polisi  ,Justine Masejo  kuhakikisha vishkwambi vitatu kati ya nane vilivyoporwa na vibaka wakati wa zoezi la uandikishaji wa Sensa ya watu na makazi,vinapatikana haraka iwezekanavyo.

Mongela amebainisha hayo katika kikao cha tathmini ya sensa ya watu na makazi iliyofanyika Jijini Arusha ambapo amelitaka jeshi Hilo kupitia kamanda Masejo  kuhakikisha vishkwambi hivyo vinapatikana licha ya zoezi hilo kukamilika kwa mafanikio makubwa mkoani hapa.

"Nimwagize mkuu wa polisi Arusha kuhakikisha  vishkwambi vitatu vilivyopotea vinapatikana haraka iwezekanavyo,kama mkoa tumefikia asilimia  100 ya zoezi la sensa ya watu na makazi'alisema.

Alifafanua kwamba uhesabuji wa majengo umevuka malengo na kufikia majengo  517,720.

Alisema kwamba changamoto ya upotevu wa vishkwambi hivyo 8 ambapo 5 vitano vimepatikana na kubakia vitatu na kuagiza jeshi la hilo mkoani hapa kuhakikisha vinapatika vyote vilivyopotea.

"Niliombe Jeshi la Polisi licha ya kupatika vishkwambi 5 hivyo vitatu vipatikana haraka iwezekanavyo Ili kuondoa dosari ndogo ndogo katika mkoa wetu kwani zoezi letu limevuka lengo Kwa asilimia zaidi ya 100 ya malengo yalipewa mkoa katika zoezi la sensa Kwa mkoa"alisema

Awali Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Missaile Musa ametoa pongezi na kuwashukuru wote walioshiriki katika zoezi hilo na kufanikisha Kwa asilimia zaidi ya mia Moja jambo ambalo Kwa Sasa limebakia awamu ya tatu ya mchakato wa zoezi hilo Taifani.

Kwa Upande wake Msimamizi wa zoezi la Sensa makao makuu  wa Arusha Omary Mdoka amesema kwamba awamu ya pili ya zoezi hilo imekamilika na wamefanikiwa Kwa asilimia 100 na zoezi hilo limefikia hatua ya tatu ya kuchakata ambayo inafanywa na ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS.

Mkuu wa wilaya ya Arumeru, mhandisi Richard Ruyangwa Kwa niaba ya wakuu wenzake. alisema kuwa wamewashukuru na kupongeza NBS na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Kwa miongozo yao na maelekezo yaliofanikisha zoezi la sensa ya watu na makazi kufanikiwa Kwa zaidi ya asilimia 100.

Alisema kwamba pamoja na mafanikio katika jambo lolote lenye watendaji wengi hapakosi changamoto ambazo amesema ni ndogondogo na hazikuathiri zoezi hilo hivyo zichukuliwe kuboresha kipindi kijacho zoezi hilo.



Ends...



Post a Comment

0 Comments