Na Joseph Ngilisho, ARUSHA
RAIS wa Mahakama ya Afrika inayoshughulika na Haki za Binadamu,Jaji Imam Aboud ,ametoa wito wa kulindwa kwa uhuru wa vyombo vya habari
na haki za binadamu,akisema bado haki hizo zinavunjwa na kuuweka mashakani uhuru wa demokrasia katika nchi nyingi za Afrika .
Jaji Aboud ametoa rai hiyo jijini Arusha katika mkutano wa mafunzo kwa majaji wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, kuhusu uhuru wa kutoa habari na utawala wa kisheria, yaliyoandaliwa na shirika la umoja wa Mataifa la Sayansi na utamaduni(UNESCO).
Alisema kuwa uhuru wa vyombo vya habari na usalama wao ni jambo muhimu linaloheshimu misingi ya utawala wa kisheria na demokrasia,hivyo majaji wanawajibu wa kuhakikisha wanahabari wanakuwa na uhuru wa kupewa habari na usalama wao katika nchi mbalimbali za afrika.
Alisisitiza kwa wanahabari kuhakikisha wanafuata misingi ya uandishi wa habari zinazoeleza uhalisia na ukweli wa jambo ili kuepuka kuleta mfarakano na machafuko ya ndani ama nchi kwa nchi.
"Mahakama za nchi katika umoja wa Afrika zinaweza kushirikiana na vyombo vya habari katika kutoa habari zinazohamasisha amani kuliko habari zeny2 kuleta mtafaruku "
Naye Rais wa Mahakama ya Afrika Mashariki( EACJ),Jaji Nestory Kayobera alisema alisema kesi zote zilizopelekwa katika mahakama hiyo zimetolewa maanuzi ila suala la utekelezaji wa maamuzi ya mahakama hilo sio jukumu lako.
Alisema katika mahakama hiyo mtu yoyote anaruhusiwa kufungua shauri bila gharama yoyote na kwamba hadi sasa mahakama hiyo ina mashauri zaidi ya 170 jambo ambalo halijawahi kutokea katika mahakama yoyote ya kimataifa.
Alisema katika kipindi cha miaka 20 EACJ imepokea kesi zaidi ya 630 .
Hata hivyo alizitaka nchi kuheshimu maamuzi ya mahakama hiyo ila akasema anaimani maamuzi hayo yanatekelezwa kwani hakuna mtu yoyote ama taasisi iliyowahi kurudi katika mahakama hiyo kulalamikia utekelezaji wa maamuzi yake.
Naye jaji wa mahakama kuu kanda ya Mbeya,David Ngunyale alisema mafunzo yanayohusu Utoaji wa Habari,Utawala wa Sheria na matumizi ya Akili Bandi yana lengo ya kujua uhuru wenye kufuata sheria ikiwa ni pamoja na uhuru wa kijieleza wenye kufuata sheria na sio vinginevyo.
Jaji Ngunyale ambaye alimwakilisha mkuu wa chuo cha uongozi wa mahakama ,Lushoto , alisema pamoja kuwepo kwa uhuru wa kupata habari lazima uhuru uwe na mipaka kwa kufuata misingi ya kisheria .
Alisema mafunzo hayo ambayo yamewajumuisha majaji,Hakimu ,wanahabari na wasajiri wa mahakama ,wataalamu wa sheria kutoka sekta mbalimbali, yatasaidia kuwajengea uwezo na uelewa katika utoaji wa habari sahihi.
Alizitaka mahakama kuhakikisha zinaweka mazingira mazuri ya kuwezesha kupata habari na wananchi kusikiliza na kupata taarifa sahihi.
Ends..
0 Comments