MZEE JELA MIAKA 30 KWA KUMTWISHA UJAUZITO MWANAYE WA KUZAA

 


BY NGILISHO TV,Kiteto.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, imemhukumu mkazi wa Kijiji cha Dongo, wilayani huyo, Yeremia Chidaka (60), kifungo cha miaka 30 jela baada ya kumkutia hatiani kwa kuzini na mwanawe wa kumzaa mwenyewe miaka 16.


Hukumu hiyo imetolea na Hakimu Mkazi Mosi Sasy leo Jumatano, Septemba 7, 2022 baada ya mtuhumiwa huyo kukiri kosa akisema hataki kuisumbua mahakama kwa kuwa aliamua kuzini na mtoto wake mwenyewe hakutaka aolewe na mtu ambaye alimwona na mahusiano naye ya karibu.


Alidai amlipomuuliza mke wake kuhusu wazo la kutaka mtoto wao asiolewe, mwanamke huyo alimweleza kwa dhihaka kama hutaki aolewe na Wakamba amuoe yeye mwenyewe jambo ambalo aliamua kuzini naye hadi alipompa ujauzito.


Alipotakiwa kujitetea, Chidaka aliomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa shetani alimpitia kutenda kosa hilo.


Mwendesha Mashtaka wa Polisi Mahakamani hapo, Wilfred Mollel akisema Jeshi la Polisi halina taarifa kama mthumiwa huyo aliwahi kufanya kosa lingine na kumwomba hakimu kumpa adhabu inayostahili.

Post a Comment

0 Comments