Na Joseph Ngilisho Arusha
Mlinzi wa kampuni binafsi jijini Arusha, Saidi Hasan mkazi wa Sanawari,anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 60, anashikiliwa na jeshi la polisi Mkoani hapa akituhumiwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita mwenye umri wa miaka 12 baada kumrubuni na kumpatia sh,200.
Akiongea na chombo cha habari baba mzazi wa mtoto huyo,Silvester Beda ambaye ninkada wa ccm, alisema kuwa aligundua kubakwa kwa mtoto wake mara baada ya kupigiwa simu na mwalimu anayefundisha dini katika kanisa analosali mtoto wake lililopo Kaloleni .
Kwa mujibu wa Beda,walimu walimkuta mtoto wake akiwa na noti ya sh,2000 na baada ya kumhoji, alimtaja mlinzi huyo kuwa ndiye aliyempatia baada ya kumfanyia kitendo hicho akimsisitiza asimwambie mtu.
Alisema aliamua kuondoka na mwanaye hadi nyumbani kwake na kuanza kumhoji kwa kina na kumwadhibu kwa fimbo na ndipo mtoto huyo alipomweleza kuwa alifanyiwa tabia mbaya na mlinzi hiyo baada ya kumwita ndani ya jengo analolinda ili ampatie sh,200.
"Mara ya kwanza mtoto alikataa kuwa hakubakwa lakini nilipoanza kumchapa alisema alifanyiwa tabia mbaya ,niliamua kumpeleka hospitalini ili kujiridhisha zaidi na baada ya kupimwa daktari aliniambia alikuwa ameingiliwa kingono"alisema.
Beda akiwa ameambatana na mwanaye ,aliamua kumfuata mtuhumiwa katika eneo lake la kazi na baada ya kufika na kumhoji mtuhumiwa alikana kuhusika ,lakini baadaye akiwa katika ofisi ya mtendaji Kaloleni alikopelekwa, aliomba waliongee jambo hilo ili lisifike mbali wayamalize,lakini mzazi wa mtoto hiyo aligoma na kuamua kumpeleka kituo cha polisi jijini hapa.
"Ninachotaka sheria ichukue mkondo wake siwezi kukubali tuyamalize wakati mtoto wangu ameathirika kisaikolojia "alisema.
Akisimulia tukio hilo mtoto huyo alisema kuwa siku ya jumapili akiwa na mwenzake wanaelekea kanisani,walipita karibu na jengo analolinda mtuhumiwa ndipo aliposilia anaitwa.
Alisema aliamua kumfuata mlinzi huyo kwa sababu amezoea kuwapatia kiasi cha sh, 200 wakati wanaelekea ama kutoka shuleni.
Alisema baada ya kuitikia wito,mtuhumiwa alimwamuru amfuate kuelekea chini ya jengo huku akiwa amemshika mkono akimvuta na kuahidi kwenda kumpatia sh,200 na alipofika chini ya gorofa alimlaza chini kwenye maboski na kuanza kumfanyia mchezo mchafu huku akiwa amemziba mdomo na macho.
"Nilisikia maumivu kidogo lakini sikuweza kupiga kelele kwa sababu alikuwa ameniziba mdomo na macho na kunifanyia tabia mbaya"alisema.
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Justine Masejo hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo.
Ends..
0 Comments