Na Joseph Ngilisho,SIMANJIRO.
MFANYABIASHARA maarufu wa madini ya Tanzanite, Mererani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Erick Peter (39) amefikishwa mahakamani akituhumiwa kumpachika ujauzito mwanafunzi wa Sekondari Tanzanite wilayani humo.
Akisoma mashtaka ya mtuhumiwa huyo mbele ya hakimu mkazi wilayani humo,Charles Uiso, mwendesha mashitaka wa serikali, Mosses Hamilton.
Alisema katika kesi hiyo namba 102 ya mwaka 2022 kuwa mstakiwa huyo ametenda kosa hilo kwa kumpa mimba mwanafunzi huyo wa kidato cha nne katika tarehe isiyotajwa kwenye mwezi Mei 2022.
Hata hivyo, mshtakiwa huyo Erick alikana kutenda kosa hilo la kumpa mimba mwanafunzi huyo alipoulizwa mahakamani hapo na hakimu Uiso.
Mshtakiwa huyo aliachiwa kwa dhamana mara baada ya kukidhi masharti ya dhamana yaliyomtaka kuwa na kudhaminiwa na watu wawili wenye bondi ya sh.milioni 2 kila mmoja.
Hakimu Uiso aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 4, 2022 itakapotajwa tena mahakamani hapo, kwani upelelezi wa kesi hiyo bado ujakamilika.
Hata hivyo Hakimu huyo aliutaka Upande wa upelelezi kuhamikisha unakamilisha vielelezo ikiwemo taarifa ya daktari na shuleni ili mshtakiwa asomewe maelezo ya awali mahakamani hapo.
Ends..
0 Comments