MBUNGE AAHIDI KUVUNJA NDOA YA BINTI WA MIAKA 15 ALIYESHAMBULIWA KWA KIPIGO NA MUMEWE


 
Na Joseph Ngilisho, LONGIDO 


Sakata la Binti mwenye umri wa miaka 15,Mesoni Kashiro Mkazi wa kijiji cha Gelailumbwa wilaya ya Longido, mkoani Arusha, aliyeolewa akiwa na umri mdogo ,limechukua sura mpya kufuatia mbunge wa jimbo hilo, dkt Steven  Kiruswa kuingilia kati na kuahidi kuivunja ndoa hiyo na kumrejesha binti huyo shuleni.

Dkt Kiruswa ambaye pia ni naibu waziri wa Madini amelaani tukio hilo na kueleza kuwa kilichofanywa na Mume wa binti  huyo kwa kushirikiana na Rafiki yake ni unyama uliopitiliza na kuahidi kurejesha mahari ya mtuhumiwa iwapo kama alilipa.

" Nimepokea  kwa masikitiko taarifa ya binti huyo kujeruhiwa vibaya  na mume wake ,nimeahidi kama atapona nitampeleka shule na kama ni mahari tutachanga warudishiwe,navitaka vyombo vya kisheria kusimamia vema suala hilo ili sheria ichukue mkondo wake alisema.

Ofisa Ustawi wa jamii wilayani Longido ,Atunagile Chisunga alisema tukio la ukatili wa shambulio na vipigo aliofanyiwa Mesoni Kashiro atahakikisha ofisi yake inafuatilia kwa ukaribu suala hilo ili mtuhumiwa afikishwe mahakamani na haki itendeke.

"Tunatajaria watuhumiwa watafikishwa mahakamani siku ya jumatatu na sasa bado wanashikikiwa katika kituo cha polisi" alisema.

Chisunga alieleza kuwa Usiku wa tarehe 21 mwaka huu,binti huyo alifikishwa katika kituo Cha afya Longido na hali yake ilikua mbaya sana hawezi kutembea Wala kusimama kutokana na majeraha ya kipigo cha  Mume wake akishirikiana na rafiki yake.

"Wilaya hii bado vitendo vya kikatili vipo ikiwemo Vipigo kwa wanawake na watoto,ndoa za utotoni pamoja na ukeketaji" alidai "alisema.

Mganga Mkuu wa halmashauri ya Longido Dkt Seleman Mtenjela alithibitisha kupokea mgonjwa huyo kutoka katika idara za kiusalama  akiwa na majeraha,na kudai kuwa anaendelea vizuri tofauti na alipofikishwa siku ya kwanza,ukatili upo Kwa watu wote watoto, wanawake na hata wanaume.

" Jukumu letu ni kumpatia matibabu ya kisaikolojia na matibabu ya kimwili,Tunafahamu watu wengi waliofanyiwa ukatili hawapo sawa kisaikolojia hivyo huotaji ushauri zaidi" alidai Dkt Mtenjela.

Katibu Tawala wilayani hapa Khamana Simba alisema serikali imesikitishwa na tukio hilo na kuahidi kutolifumbia jicho huku akisisitiza kuwa tukio hilo litakua la Mfano wilayani hapo Kwa wale wote wenye desturi ya kufanya ukatili kwa watoto na wanawake.

"Vyombo vya ulinzi vipo makini watuhiwa wapo kwenye mikono ya kisheria (Polisi) taratibu nyingine zinaendelea"alisema Simba.

Ends....

Post a Comment

0 Comments