BY NGILISHO NEWS, MANYARA
Vijana 8 wa jamii ya kifugaji ya Maasai, Kiteto mkoani Manyara, waliomshambulia kwa marungu Askari wa Jeshi la Polisi Kata ya Njoro, Inspekta Patrick, wamehukumiwa kwenda jela miezi sita ama kulipa faini ya shilingi elfu 50 na fidia ya laki 1 kwa kila mmoja.
Vijana walikuwa wanashtakiwa kwa makosa mawili, ambapo kosa la kwanza ni kumshambulia Askari Polisi wa Kata ya Njoro A/ Inspekta Patrick aliyeitwa kusaidia kuondoa mifugo iliyokuwa inakula mazao shambani, na shtaka la pili ni kumpiga Askari Mgambo waliokuwa na Askari huyo katika tukio hilo.
Hakimu wa Mahakama ya wilaya ya Kiteto, Boniface Lihamwike, alipowauliza watuhumiwa hao kuhusu madai ya makosa hayo mawili, watuhumiwa walikiri makosa kuwa waliyatenda wao wenyewe.
Mwendesha mashtaka Salimu Issa Bakari aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Alangai Manywele, Elenyoki Manywele, Lazaro Mbuki, Kamunga Mbuki, Mteriani Mbuki, Mukara Ngurdada, Moita Taleck na Kilesii Alli
Hakimu Boniphasi Lihamwike Aliwauliza watuhumiwa kama wana cha kujitetea ambapo waliiomba Mahakama iwapunguzie adhabu huku wakisema kuwa hilo ndio kosa lao la kwanza na pia wanategemewa na familia.
Hata hivyo washtakiwa hao kwa pamoja walilipa faini hiyo.
Chanzo - EATV
0 Comments