Na Joseph Ngilisho Arusha
Kamati ya Kudumu ya bunge, huduma na Maendeleo ya jamii,imeridhishwa na hatua ya ujenzi wa jengo la Ufundi Tower uliofikia asilimia 99, katika chuo cha ufundi Arusha na kuagiza mradi huo ukamilike kwa wakati ili liweze kupokea wanafunzi ifikapo mapema mwezi oktoba mwaka huu.
Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Stanslaus Nyongo wakati kamati hiyo ilipotembelea chuo cha Ufundi ATC Jijini Arusha.
Alisema kwamba kamati hiyo imeridhishwa na matumizi ya fedha za uviko 19 kiasi cha sh,bilioni 1.7 zilizotolewa na serikali kwa ajili ya kumalizia kutekeleza mradi huo unaogharimu thamani ya sh, bilion 5. 694
"Tumeona thamani halisi ya fedha zimerumika ipasavyo, tunapongeza ila tunatoa rai kwa wale wote wanaopewa utekelezaji wa miradi kujenga au kutekeleza kwa thamani halisi itakayosaidia kuokoa fedha za umma na wajue zama zimebadilika waache kutekeleza chini ya viwango "alisema.
Katika hatua nyingine kamati hiyo ilitembelea chuo cha Ualimu, Elimu maalumu, Patandi kukagua ujenzi wa bweni la wanawake lenye uwezo wa kuchukuwa wanafunzi 80 ambalo limekamilika kwa asilimia 100 lenye thamani ya milioni 187 fedha za UVICO-19.
Akiwa chuoni hapo Mwenyekiti wa kamati hiyo ameitaka wizara ya Elimu kupeleka fedha za kuweka sakafu ya marumaru badala ya sementi iliyowekwa ambayo haiendani na hadhi ya jengo hilo.
"Sisi kama kamati tumeridhika na matumizi ya fedha za serikali katika ujenzi wa bweni hilo kwa thamani halisi ya fedha zilizotumika na limekamilika kwa viwango bora "alisema
Mwenyekiti Nyongo alitoa rai kwa kuiomba serikali kuhakikisha inaongeza jitihada zaidi katika kuimarisha na kuboresha miundombinu kwenye vyuo na shule zake ili kuweka mazingira mazuri ya kujifunzia na kufundisha.
Awali akiongea Mbele ya kamati hiyo Mkuu wa chuo cha Ualimu Elimu Maalum Patandi Lucian Segesela alisema Mradi huo umekuwa ni faraja kubwa kwa wanapatandi na Tanzania kwa Ujumla na msaada kwa watu wenye ulemavu na umeongeza udahili kutoka wanafunzi 430 hadi kufikia wanafunzi 518
Alisema kwamba changamoto kubwa ni kuendelea kuongeza majengo ili kuweza kuongeza udahili mkubwa kwa wanafunzi
Kamati hiyo pia imetembelea Tume ya Taifa ya nguvu za Atomu TAEC na kuridhishwa na ujenzi wa jengo la maabara na madarasa ya mafunzo rmradi wenye thamani ya bilioni 10.977 ambao umefikia asilimia 97 jengo hilo litasaidia kuzalisha wataalamu wa nyanja ya teknolojia ya nyuklia katika sekta za Afya kilimo barabara maji na mifugo.
Akiongea Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof.Lazaro Busagala alisema kwamba ujenzi wa maabara hiyo utakapokamilika utaongeza ufanisi katika eneo la utekelezaji wa Sera ya Taifa ya viwanda kwa teknolojia ya nyuklia ambapo kwa sasa kuna zaidi ya vituo 80 vinavyotumia vifaa vya mionzi viwandani.
Awali akiongea baada ya kutembelea jengo hilo Mwenyekiti wa kamati hiyo Stanslaus Nyongo amesema kwamba wameridhirishwa na ujenzi wa jengo hilo na umelingana na thamani halisi ya fedha zilizotolewa na serikali na unaufanisi wa hali ya juu ambapo wanatambua umuhimu wa suala la mionzi katika matumizi salama ya viwandani na binadamu.
Ends....
0 Comments