JESHI LA POLISI LAWAFUKUZA KAZI KWA FEDHEHA ASKARI WAKE WATATU ARUSHA


Na Joseph Ngilisho,Arusha

 
Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha,Kamishina Msaidizi,Justine Msejo alsema kuwa jeshi hilo limewafukuza kazi askari kwa fedheha askari wake watatu kwa kosa la kwenda kinyume na maadili ya jeshi hilo katika tukio ambalo hakuwa wazi.
 
Msejo akiongea ofisini kwake aliwatahadharisha askari polisi Mkoani Arusha wanaoenda kinyume na maadili yao kuwa yatawakuta haya yaliyowakuta wenzao.

Aliwataka kufanya kazi kwa kufuata msingi ya kazi ikienda sambamba na weledi wa kazi na wenye tabia ya kukiuka misingi ya kazi sheria ipo na hawatahurumiwa na mkono wa sheria utawakuta dhidi yao.
 
Alisema askari hao watatu kwa nyakati tofauti wamebainika kwenda kinyume na maadili ya kazi ya jeshi la polisi ikiwemo kushindwa kuzingatia nidhamu, haki, weledi na uadilifu katika utendaji kazi hivyo hawatoshi kuwa katika jeshi hilo.
 
"Hao askari tumewaondoa katika jeshi letu na tutaendelea kufuatilia na wengine watakaoshindwa kufanya kazi kwa uadilifu, kulingana na kiapo walichokikubali wakati wanajiunga na jeshi hilo,” alisema Masejo
 
"Niwatake askari wengine wenye tabia kama hizo kama wanataka kuendelea na kazi ya kulitumikia jeshi la polisi basi wahakikishe wanafuata nidhamu na maadili ya kazi," amesema
 
Kamanda huyo alisema kwa sasa hawezi kuweka wazi majina ya polisi waliofukuzwa katika jeshi hilo kwani bado upelelezi unaendelea wa kuwachunguza askari wengine na wataendelea kuchukuliwa hatua za kinidhamu na wale watakaobainika kuvunja sheria za nchi basi watawafikisha katika mikono husika.
 
Katika siku za Karibu Mkoani Arusha kulitokea matukio mawili ya Polisi kuomba rushwa moja likiwa la Kwa Mrombo Jijini Arusha la askari watatu kuomba rushwa ya shilingi milioni 3 na kurudisha shilingi milioni 2.5 na lingine likihusisha askari wanne wa Kituo cha Polisi Ngaramtoni kwa kuomba rushwa ya shilingi milioni 6 na baadae kurudisha ofisini kwa Kamanda Masejo.
 
Katika tukio la kwanza askari walihusika ni pamoja na Maofisa Wakaguzi Wasaidizi Watatu wa Polisi  Arusha akiwemo Mkuu wa Kituo cha Polisi Engutoto ,Mkaguzi Msaidizi Mahamud Jakaya kwa kosa la kupora zaidi ya shilingi mlioni 3 za Mfanyabiashara wa Mazao, Ramadhani Hamisi  kutoka Mkoani Dodoma aliyedaiwa kufanya biashara ya Mirungi.
 
Wengine waliohusika katika tukio hilo ni pamoja na Mkaguzi Msaidizi ,Ramadhani Mcheka na Mkaguzi Msaidizi aliyetambulika kwa jina moja la Machanganya ambao wote wawili ni askari viongozi kitengo cha Polisi Jamii katika wilaya ya Arusha.

Tukio la pili lilihusisha askari wanne wa Kituo cha Polisi Ngaramtoni ambapo walikiri kupokea shilingi milioni 6 mbele ya Kamanda Msejo kutoka kwa mfanyabiashara mwenye asili ya Kisomali aliyedaiwa kusafirisha dola zenye thamani ya shilingi bilioni Moja kutoka Namanga kwenda Jijini Arusha.

Matukio yote hayo Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha amekuwa mgumu kuyatolea maelezo pindi anapohitajika na kueleza kuwa yanachunguzwa na kwenda mbali zaidi kusaka askari polisi wanatoa taarifa za matukio hayo kwa waandishi wa habari.

Ends...


Post a Comment

0 Comments