Na Joseph Ngilisho, ARUSHA
MBUNGE wa Arusha Mjini Mrisho Gambo amesema hatishiki na mchezo mchafu unaofanywa na baadhi ya viongozi wa chama chake cha ccm mkoani hapa dhidi yake, kumdhoofisha kisiasa akidai wamejaa unafiki na usaliti dhidi yake katika mapambano ya mafisadi.
Gambo ametoa kauli hiyo kali wakati akiongea na wafanyabiashara wa soko la Krokoni jijini hapa,alipoenda kukabidhi Matofari na mabati kwa ajili ya ujenzi wa choo katika soko hilo.
Alieleza kwamba kamwe hatarudi nyumba katika kupambana na ulaji wa fedha za umma katika halmashauri ya jiji la Arusha hata kama atabaki peke yake katika mapamvao hayo .
"Wapo watu wachache hapa Arusha ambao wameweka genge lao kwa ajili ya kupiga dili na kufanya ufisadi na wizi wa fedha za halmashauri yetu ,suala ambalo nimelikataa "
Aliongeza kuwa wapo baadhi ya watu wanasema mbunge haelewani na viongozi wenzake nataka wananchi wenzangu waelewe hata ashuke nani hapa hatuwezi kuelewana na watu wanaotetea wezi
"Jimbo la Arusha mjini sio jepesi ni jimbo la watu wanaojielewa itafika mahala wananchi wataamua kuchagua mtu na sio chama "alisema Gambo
Akatolea mfano kwamba kuna mtu ameenda halmashauri (akimaanisha Dkt John Pima)na kuiba fedha kiasi cha sh, milioni 103 ,akasema badala ya kuungana tutetee maslahi ya umma lakini wapo watu wanaungana kutetea mafisadi.
Alisema wapo viongozi wa serikali na chama mkoani hapa wanaenda magereza kumtembelea mhalifu (Dkt Pima)ambaye ameihujumu na kuibia serikali .
"Wakati rais Samia anapambana na ufisadi kwenye nchi ,anapambana kutafuta fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo , serikali yake inawakamata wahalifu lakini Leo hii wapo viongozi katika mkoa huu wanamtembelea mhalifu gerezani "alisema
Aliongeza kuwa kitendo kama hicho kinachofanywa na viongozi hao ni kuidharau serikali na mamlaka zake inayopiga vita dhidi ya ufisadi.
Gambo aliapa kuendelea kupingana hadharani na viongozi wa namna hiyo ambao wamejikita kuendeleza wizi na ufisadi ila atashirikiana na viongozi wenye nia njema na jimbo la Arusha mjini .
Alisema watu wote wanaosimamia haki wamekuwa na misukosuko mingi na yeye kama mbunge wa miaka mitano akisimamia wezi na kulinda maslahi ya wananchi na kusema kuwa hatakaa chini kamwe kumsujudia mtu ili awasaliti wananchi.
Alionya kikundi cha watu wachache ndani ya ccm wanaoendelea kumpiga vita, kamwe hakitashinda yeye ni mbu ge wa wananchi na ataendele kusimama na wananchi .
Alisema kwamba mtu anayeamini mbunge akiwa mstari wa mbele kupambana na ufisadi na wezi itakuwa ni sababu ya kukosa ubunge mimi kwangu hilo halinitishi miaka mitano inatosha kabisa na mwaka 2025 ikifika wananchi wataamua.
Ends
0 Comments