Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini,Willibroad Mtafungwa |
BY NGILISHO NEWS :KAHAMA
Watu 16 wamefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa katika ajali mbaya iliyohusisha magari matatu ikiwamo trekta iliyotokea eneo la Mwakata Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Hata hivyo katika eneo la ajali shughuli za uzalishaji zilisimama kwa zaidi ya saa nne wakati waokoaji wakinasua miili ya merehemu iliyokuwa imenaza kwenye magari ya ajali.
Ajali hiyo imetokea Saa 4:00 usiku wa kuamkia leo Jumanne, Agosti 9, 2022 ikihusisha gari ndogo aina ya IST, Hiace na Lori.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Kahama, Dk Deogratius Nyaga amethibitisha kupokea miili ya watu 20 na majeruhi 15 wanaoendelea kupatiwa matibabu.
Kaimu Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Shinyanga, Leonard Nyanduhu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, amesema uchunguzi unaendelea.
0 Comments