VIBAKA WAKWAPUA VISHKWAMBI VYA MAKARANI WA SENSA ARUSHA

 

Zoezi la sensa ya Watu na Makazi jijini Arusha,limeingia dosari kufuatia   makarani wawili kujikuta katika wakati mgumu  baada ya watu wanaodaiwa kuw ni vibaka wasiojulikana katika eneo la Unga limited kuwapora vifaa vyao vya kukusanyia taarifa maarufu kama vishikwambi .


Tukio la kwanza limetokea jijini Arusha ambapo karani aliyetambuliwa kwa jina la Saraphia Kiwango ameporwa kishikwambi chake alipokuwa akielekea kuanza kuhesabu makundi maalum katika Kata ya Unga Ltd jijini hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 23, Diwani wa Unga Ltd, Mahmoud Said amesema alipokea taarifa usiku wa kuamkia Agosti 23, kuwa kuna karani ameibiwa kishikwambi na mumewe kujeruhiwa kichwani na bodaboda hao wawili.

"Jana usiku hawa makarani wa Sensa waliitwa kwa mtendaji wakati wanakwenda huko ndiyo wakakutana na vibaka waliokuwa kwenye bodaboda wakamjeruhi mumewe na kumpora kishikwambi kisha kutoweka kusikojulikana," amesema.

Mtendaji wa Kata hiyo, Sophia Laizer amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa karani huyo baada ya kuibiwa kishkwambi hicho na kuwa alivamiwa na vijana hao akiwa njiani kuelekea kuhesabu makundi maalum.

"Ni kweli tukio hilo lilitokea jana usiku lakini ameshapewa kishkwambi kingine na anaendelea na kazi,"  kwa amani.


Naye Mratibu wa sensa wilaya ya Arusha, Maneno Maziku amekiri kutokea kwa tukio hilo ila kitu kiko sawa na kuwa aliyejeruhiwa anaendelea vizuri na kuwa kayika maeneo mengine zoezi linaenda vizuri.

"Ni kweli aliporwa kishikwambi na mume wake kujeruhiwa kichwani lakini ameshapewa kishikwambi kingine anaendelea na kazi lakini pia majeruhi hali yake inaendelea vizuri," amesema bila kuwataja majina yao.

Hata hivyo, akizungumzia kazi hiyo Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Said Mtanda amesema hali ni shwari katika maeneo mengine na kuwa watakaotaka kuvuruga sensa.

"Hali ni shwari ila jana usiku kuna karani mmoja wahuni walitaka kumshambulia kwa sababu tuliweka mgambo na polisi walidhibitiwa," amesema.


Post a Comment

0 Comments