UCHAGUZI CCM NGARENARO HOFU TUPU ,DIWANI AHUSISHWA


Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

Baadhi ya wagombea na wanachama wa chama mapinduzi kata ya Ngarenaro wameonesha kuwa na wasiwasi katika uchaguzi wa viongozi wa kata hiyo unaotarajiwa kufanyika hapo kesho , baada ya kuwepo taarifa kwamba kuna baadhi ya mamluki wamepandikizwa kuvuruga uchaguzi huo .

Wanachama hao wameibuka na kudai kuwa hawana imani na uchaguzi huo baada ya majina ya viongozi wanaowahitaji kukatwa wakimtuhumu diwani wao,Isaya doita kuingilia uchaguzi huo.

Wakiongea na vyombo vya habari baadhi ya wanachama hao wamemtuhumu diwani wa kata hiyo,Isaya Doita kwa kuendesha siasa za makundi  na kushawishi majina ya wagombea wa nafasi ya umwenyekiti kukatwa kwa maslahi yake.


Wanachama hao ambao waligombea nafasi mbalimbali na baadhi yao majina  kukatwa,Yusuf Sharif ,Leonard  Lema na Philip   Mtui wamedai kuwa diwani huyo ameingilia uchaguzi huo kwa  kiasi kikubwa kiasi cha kutamka wazi kwamba viongozi waliokatwa wamepoteza mvuto wa kisiasa.

Yusuph  sharif ambaye aligombea nafasi ya ukatibu kata alisema kuwa baadhi ya wanachama ambao sio wakazi wa kata ya Ngarenaro ,wameletwa na diwani Doita katika kata hiyo kushiriki uchaguzi jambo ambalo walidai hawana imani na uchaguzi huo.


Naye Philip Mtui alisema uchaguzi wa kata ya Ngarenaro  umeingiliwa tangu ngazi ya matawi na kuna watu wamepandikizwa na diwani huyo na amekuwa akionesha wazi wagombea anaowahitaji jambo ambalo linasababisha kupoteza baadhi ya viongozi makini kwa kuletewa mamluki.

Alisema kuwa malalamiko yao wameyafikisha ngazi ya katibu waccm wilaya lakini walijibiwa kuwa wasubiri kwanz uchaguzi ukamilik ili waweze kuleta malalamiko yao ofisini.

Akiongelea tuhuma hizo diwani Isaya Doita alikanusha vikali kuhusika na uteuzi wa wagombea na kuelez kuwa yeye sio anayehusika na uteuzi na hao wanaolalamika tuhuma zao  hazina mashiko wanapaswa kupuuzwa .

Doita alienda mbali zaidi kwa kudai kuwa wanaolalamika wamepoteza mvuto wa kisiasa na wasitafute mchawi bali waangalie ni wapi walipojikwaa.


Jitihada za kumpata katibu wa ccm wilaya ya Arusha Kataba Sukuru ili kuzungumzia mwenendo wa zachaguzi mbalimbali kwenye kata zinaendelea.







Post a Comment

0 Comments