Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Taasisi ya uhandisi na usanifu mitambo nchini (TEMDO) imebuni mtambo mpya wa kisasa wa kuchakata mafuta ya alizeti ambayo yatasafishwa katika ubora kwa kiwango cha juu kwa ajili ya matumizi ya binadamu.
Taasisi hiyo imeutambulisha mtambo huo kwa mara ya kwanza katika maonyesho ya sikukuu za wakulima nchini (Nane Nane) yanayoendelea katika viwanja vya Nanenane eneo la Njiro jijini Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa kitengo cha mawasiliano na masoko katika taasisi hiyo,dkt Sigisbert Mmasi alisema kwamba mtambo huo mbali na kuchakata mafuta ya alizeti lakini utayasafisha mafuta hayo na kisha kutawekea virutubisho.
Alisema kwamba mtambo huo utasaidia kusafisha mafuta ghafi ya alizeti ambayo yana athari kwa afya ya binadamu na kuyasafisha katika ubora huku akiwataka wakulima kuwekeza katika mtambo huo kwa manufaa ya biashara zao.
Mbali na mtambo huo mitambo mingine iliyobumiwa na taasisi hiyo ni ,mtambo wa kuchakata Sukari,mtambo wa kukamua mafuta ya Parachichi,Kiteketezi xha kuchoma taka za hospitalini ,vifaa tiba kama vitanda ,stand ya drip na jokofu la kuhifadhia maiti.
"Tumekuja nanenane kuwaonyesha wamulima huu mtambo wa kuchakata mafuta ya alizeti hivyo mtambo huu utawasaidia wakulima nawaomba wawekeze kwenye huu mtambo"alisema Mmasi .
Awali mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango alizitaka taasisi za kilimo kubuni zana mbalimbali zitakazowasaidia wakulima katika shughuli zao na aliipongeza taaisisi ya Temdo kwa ubunifu wa mitambo mbalimbali itakayosaidia maendeleo ya kilimo, mifugo na uvuvi nchini .
Aliyasema hayo jijini Arusha ,kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Arusha wakati akifungua maonyesho ya kilimo na mifugo nanenane yenye kauli mbiu ya"agenda 10/30 kilimo ni biashara ,shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo,mifugo na uvuvi".
Alisema kuwa, maonyesho hayo yanatarajiwa kuchangia ukuaji wa mabadiliko kwa wakulima kutoka maeneo mbalimbali endapo elimu ya kutosha itatolewa na kuenea kwa elimu kwa jamii inayowazunguka juu ya killimo na ufugaji wa kisasa .
Aidha aliwataka watalaamu wa kilimo nchini kuendelea kutoa elimu ya kutosha kwa wakulima na wafugaji ili walime na kufuga kisasa na kuepukana na kuondokana na zana za zamani na hatimaye kuweza kubadilisha maisha yao.
Naye Mkuu wa wilaya ya Kiteto ,Mbaraka Alhaji Yusuph alisema kuwa,maonyesho hayo yameshirikisha waonyeshaji 200 kutoka Taasisi mbalimbali licha ya taarifa kuchelewa juu ya uwepo wa maonyesho,lakini mwitikio bado ni mkubwa sana.
Ends...
0 Comments