SENSA YA WATU NA MAKAZI KESHO,DC AONYA VIKALI

Na Joseph Ngilisho Arusha 

Wakati zoezi la Sensa ya watu na makazi likitarajiwa kuanza hapo kesho,mkuu wa wilaya ya Arusha,Saidi Mtanda amepiga marufuku kwa makarani  na wote watakao ambatana  katika zoezi hilo, kuvaa mavazi yenye mlengo wa vyama vya siasa ili kuepusha kutia dosari zoezi hilo.

Akiongea na waandishi wa habari mapema leo ofisini kwake,amesema kuwa maandalizi ya zoezi hilo wilayani humo yamekamilika ,na hatua ya kwanza ya dodoso la kuhesabu linatarajia kuanza saa 6.01 usiku kwa  makundi maalumu yakiwemo ya watoto wa mtaani na waliolala hotelini na nyumba za kulala wageni.

Alisema kuwa zoezi la Sensa halina itikadi ya kisiasa ,kidini wala kikabila na kuwataka makarani wa Sensa kutodhubutu kuvaa vazi lolote linalotambulisha chama cha siasa.

Mtanda alisema kuwa zoezi la sensa kimkoa litazinduliwa leo majira saa sita usiku na mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongela katika makumbusho ya mnara wa Azimio la Arusha, ambapo pamoja na mambo mengine atafyatua fataki maalumu kama ishara ya uzinduzi.

Alifafanua kuwa zoezi la uhesabuji watu litaanza mapema agosti 23 hadi agosti 28 na Agosti 29 makarani wa Sensa wakiwa wameambatana na  wenyeviti wa mitaa na watendaji wataendelea na dodoso la majengo hadi septemba 6 litakapofungwa rasimi zoezi hilo.

Aliwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa makarani  wa Sensa ili kufanikisha zoezi hilo .

Aidha amelitaka jeshi la polisi mkoani hapa,kuhakikisha linaimarisha ulinzi na usalama hasa katika uzinduzi wa zoezi hilo .
Ends....











Post a Comment

0 Comments