BY NGILISHO TV
Mtoto mwenye umri wa miaka 12 mkazi wa Kitongoji Cha Mringa Kata ya Olorien Wilayani Arumeru Mkoani Arusha Brayson Vumilia amefariki dunia kwa kujinyonga kwa kutumia mtandio wa kanga ya mama yake mzazi ambapo mpaka Sasa Chanzo Cha kifo hicho hakijajulikana .
Akizungumzia tukio Hilo mwenyekiti wa Kitongoji Cha Mringa Noel Saning'o amesema kuwa tukio Hilo limetokea Jana majira ya SAA tatu usiku ambapo Mtoto huyo alikuwa amejifungia kwa ndani baada ya mama yake mzazi kwenda kununua mboga aliporudi akagonga mlango na kukuta haufunguki alipochungulia dirishani akaona Mtoto wake amejining'iniza kwa kutumia mtandio.
0 Comments