BY NGILISHO NEWS .
Wiki moja baada ya kufunguliwa kwa pazia la ubunge wa Afrika Mashariki (EALA), wanachama 64 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamejitokea hadi leo Alhamisi, Agosti 4, 2022 kuomba ridhaa ya kuwania nafasi hiyo.
Idadi hiyo inaashiria mchuano mkali katika kinyang’anyiro hicho, kinachohitaji watu tisa wakiwemo wawakilishi kutoka vyama vya upinzani.
Miongoni mwa makada wa chama hicho waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi hizo ni Godfrey Shirima, Dk Paul Anthony, Henry Bulengera na James Kasurura.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Oganaizesheni, Maudline Castico amewataja wengine ni Nasikiwa Berya, Amina Mgeni, Ambwene Kajura, Nasser Nzamba, Prakseda Marmo, Maria Kangoye na Shogo Mlozi.
“Yupo Alfa Munyi, Manase Michael, Ayubu Lemilya na Nicksoni Kahimba waliochukulia Dar es Salaam, huku Haji Vuai Ussi, akichukua kwa upande wa Zanzibar,” amesema.
Kwa mujibu wa Castico, milango ya kuchukua fomu za kuwania nafasi hizo itakuwa wazi hadi Agost 10, 2022.
0 Comments