IMMAM MKUU WA MSIKITI WA ZAHRA, SHEIKH MAULID SOMBI |
Na Joseph Ngilisho ARUSHA
WAUMINI wa madhehebu ya SHIA, mkoa wa Arusha,wameadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hussein,mjukuu wa Mtume Muhamada ,kwa kutoa tamko la kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassani katika kuhakikisha watanzania wanapata huduma ya maji,dawa, na damu kwenye hospitali mbalimbali.
Sambamba na hilo wameiomba serikali kuongeza jitihada za kupiga vita vitendo vya ukatili kwa watoto ambavyo vinashamiri kwa kiasi kikubwa pampa na mauji ya kutisha.
Hayo yameelezwa na Imamu mkuu wa msikiti wa Zahra mkoa wa Arusha, Shekhe Maulid Hussein Sombi,kwenye maadhimisho ya siku ya Ashura,ambayo ni kumbukumbu ya kifo cha Imamu Husseini mjukuu wa Mtume Muhamad aliyeuawa na mtawala dharimu, Yazid bin Muawiyah,kwenye mji wa Karbala,nchini, Iraq
Katika maadhimisho hayo yaliyoenda sanjari na uchangiaji wa damu na kutoa misaada ya vyakula na maji kwa makundi yenye uhitaji ,Imami Sombi alisema hawataki kuona watu wanaishi katika ugomvi ,matusi bali waishi kwa amani na kupata huduma muhimu za kijamii .
Amesema kuwa katika maadhimisho hayo ambayo yameanza Augosti mosi na yatafikia kilele chake Augosti 13,wamechangia chupa 58 za damu,ambazo tayari wameshazikabidhi kwa uongozi wa hospitali ya mkoa ya Mount Meru pia wametoa misaada ya vyakula na maji ya chupa kwa watu mbalimbali
Shekhe,Maulid,amesema kuwa lengo la maadhimisho hayo yaliyoathimishwa kwa maandamano ya amani ya kutembea bila viatu ni kupinga ukatili,manyanyaso ,uonevu kufanyiwa kwa mtu yeyote na badala yake kujenga upendo ,mshikamano na umoja bila ubaguzi na wanalaani tukio hilo lakuuliwa Imamu Hussein.
Kuhusu Sensa ya watu na makazi itakayofanyika Augosti 23 mwaka huu,amesema waumini wote wa dhehebu la Shia,mkoa wa Arusha,watashiriki kwa kuwa Sensa ina faida nyingi ambazo zinaiwezesha serikali kufahamu Idadi ya watu wake na kutoa huduma nzuri kulingana na mahitaji hivyo wao watashiriki kwenye Sensa.
Amesema bila Sensa serikali haiwezi kutekeleza mipango yake ipasavyo Sensa ni jambo la ,muhimu sana ili kuweze kupatikana kwa huduma bora zinazotosheleza lazima kolakitukufahamike idadi yake
Shekhe, Maulid,amesema Imam Hussein aliuliwa mwezi mtukufu wa Muharram,siku ya Ashura, akiwa na wafuasi 82 wakiwemo wanawake,watoto,Yatima na wajawazito tukio hilo la kikatili na kinyama, limekuwa ni la kihistoria hivyo wanabeba ujumbe wa mshikamano upendo na ushirikiano kuishi bila ubaguzi
Naye maalimu wa Chuo cha Ahlul bait centre,Shekhe Muhamad Hashim,amesema wanaadhimisha kifo cha mjukuu wa mtume Muhamad S.A.W ,Ikiwa ni hatua ya kuelewesha ulimwengu ubaya wa tukio hilo ili ukatili wa aina hiyo usije ukajirudia kwa wengine na. wanalaani tukio hilo.
Ends.
0 Comments