Na Joseph Ngilisho Arusha
Msiba wa mtoto wa Tajiri maarufu jijini Arusha, Meckline Temu (DENSO) aliyefiwa na mwanaye,Estomi Temu , kwa ajali mbaya ya gari akiwa na mpenzi wake, Nice Mawalla(24)umegeuka kituko kufutia genge la wahuni kuibuka katika msiba huo ,wakiwa wamelewa na kupokonya kamera za waandishi wa habari .
Marehemu hao Nice na Estomi wanaodaiwa ni wachumba walifariki dunia papo hapo kwa ajali mbaya ya gari juzi majira ya saa saba na nusu usiku katika eneo la Ngulelo, jijini hala wakidaiwa kutoka Klabu na katika tukio hilo Nice alipasuka kifua na kuvunjika mkono wa kulia na Estomi akiumia kwa ndani na kutokwa na damu puani na masikioni.
Katika msiba huo ambao umetawaliwa na magari ya kifahari yasiyo na idadi,umegeuka sherehe kutokana na idadi kubwa ya pombe za kila aina kufurika nyumbani kwa tajiri huyo .
Magari ya waombolezaji ambayo ni ya matajiri katika jiji la Arusha na Moshi,yamefunga mtaa na kuibua kero kwa wananchi waliopo karibu na eneo la msiba nyumbani kwa tajiri, Kwa Mrefu jijini hapa, baada ya kukosa eneo la maegesho na kupelekea magari hayo kuegeshwa barabara kuu ya Arusha Moshi.
Nyumbani kwa Tajiri vijana mbalimbali sanjari na wazee walionekana wakiwa katika makundi makundi wakipata vinywaji huku wengine wakihamishia kambi msibani hapo mpaka asubuhi.
Estomi na Nice walifariki dunia juzi saa 7.30 usiku eneo la Kwa Ngulelo wakiwa kwenye gari la kifahari aina ya Ranger Rover lenye namba T 313 AUH ambalo limeharibika vibaya ,baada ya kuacha njia na kupinduka likiwa kwenye mwendo kasi.
Waandishi mbalimbali wa habari walitia timu katika msiba huo kupata habari lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida walikutana na shibiri ambapo mwandishi wa Milard Ayo ,Godfrey Thomas alinusurika kuvunjiwa kamera yake huku memory Kadi ikivunjwa vunjwa na kundi la wahumi wakiongozwa na baadhi ya wanandugu akiwemo kaka wa marehemu,Brighton Temu na Kelvin Masuwa.
"Hawa Ndugu hawakutaka tuchukue picha ndio maana wali nipokonya kamera na kuharibu Kadi yangu ,nimepoteza kazi nyingi zilizokuwa kwenye kadi"alisema Godfrey Thomas.
Taarifa kutoka ndani ya familia zimeeleza kuwa marehemu Estomi anataraji kuzikwa siku ya ijumaa jijini Arusha huku taratibu za maandalizi zikiendelea.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine hakuwa tayari kuzungumzia tukio hilo licha ya waandishi wa habari kumpigia simu mara kadhaa.
''Sina taarifa za tukio hilo labda nifuatilie "ni kauli ya Kamanda pale alipokuwa akipigiwa simu na waandishi wa habari wakitaka kujua chanzo cha ajali.
Hata hivyo taarifa kutoka ndani ya familia hiyo zinadaiwa kuwa baba wa marehemu DENSO hakutaka taarifa za msiba wa mwanaye ambaye ni mtoto wa mwisho kutangazwa kwenye vyombo vya habari ukizingatia tukio hilo lina mhusisha na masuala ya ulevi .
Shuhuda wa tukio hilo ambaye hakuwa tayari jina lake kuandikwa gazetini alisema kuwa baada ya tukio hilo watu waliojidai ni wasamalia wema walivamia gari hilo na kupora kila kitu cha thamani mali za marehemu hao zikiwemo simu na fedha.
Ends...
0 Comments