BY NGILISHO TV
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura amefanya mabadiliko madogo kwa baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa nchini.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 12, 2022 na Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP David Misime.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, IJP Wambura katika mabadiliko hayo amemuhamisha Kamishna Msaidizi wa Polisi,ACP Pili Omary Mande ambaye alikuwa Afisa Mnadhimu Namba Moja Mkoa wa Ruvuma kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi.
ACP Mande anachukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Marco Godfrey Chillya ambaye anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma akichukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Joseph Konyo ambaye amestaafu.
Wakati huo huo, IJP Wambura amemhamisha aliyekuwa Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Gaudiunus Felician Kamugisha kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja akichukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Abdallah Haji Seti aliyehamishiwa makao makuu ya Polisi Zanzibar.

0 Comments