Na Joseph Ngilisho Arusha
Halimashauri ya Arusha(Arusha Dc) wilayani Arumeru imemtunuku cheti cha Shukrani,Mfanyabiashara Maarufu, dkt Philemon Mollel(MONABAN)baada ya kutambua mchango wake katika kuchangia miradi ya maendeleo iliyozinduliwa na mbio za mwenge wa uhuru juni 22 mwaka huu.
Akikabidhi cheti hicho katika baraza la madiwani la halmashauri hiyo,Mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Seleman Msumi alisema kuwa halmashauri hiyo inatambua na kuthamini mchango wa wadau wa maendeleo ndio maana imeamua kuwashukuru kwa kuwapatia cheti maalumu cha heshima ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao.
Alisema Mollel na wenzake 10 walisaidia kufanikisha mbio za mwenge wa uhuru katika halmashauri hiyo ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya sh,bilioni 4.2 ilizinduliwa .
"Katika ujio wa mwenge wa uhuru tuliweza kushirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo ambao walituchangia vifaa vya ujenzi na fedha thasilimu, ambapo Dk Philemon alifanikiwa kutupatia mifuko 60 ya saruji kwa ajili ya kumalizia shule ya sekondari Oldadai,na hivyo kwa kutambua mchango wake tukaona ni busara kwa halmashauri kumkabithi vyeti vya shukrani."alisema Msumi.
Kwa upande wake,mfanyabiashara Mollel ambaye pia ni Askofu wa kanisa la Kilutheri la Afrika Mashariki(KKAM),ameshukuru baraza hilo kwa kutambua mchango wake na kukumbuka fadhila kwa kumkabithi cheti cha shukrani jambo ambalo linatoa motisha wa kuendelea kusaidia zaidi.
Dk.Mollel alisema kuwa,kitendo kilichofanywa na halmashauri hiyo ni jambo kubwa na linahitaji kuigwa na taasisi zingine ili watu waendelee kuwa na motisha wa kuisaidia jamii katika maswala mbalimbali.
"Mimi niseme tu nimefurahishwa sana kwa zoezi hili na kipekee naahidi kuendelea kusaidia zaidi katika maswala mbalimbali ya maendeleo ili jamii yetu iweze kusonga mbele na kuondokana na changamoto mbalimbali. "alisema Mollel.
Wengine waliohudhulia zoezi hilo na kukabidhiwa cheti ni pamoja na Elibariki Kiberenge na Eliaman Mollel.
Ends...
0 Comments