Mwanamke mmoja,Irene Shaban mkazi wa Sokoni One jijini Arusha,anaugulia maumivu makali baada ya kuvunjwa meno yake ya mbele kwa kipigo cha mume wake ,Zuber Mbonea ambaye ni Dereva bodaboda, baada ya kijana huyo kuuliza chakula na kujibiwa hakijapikwa kwasababu hakuacha pesa.
Akiongea kwa taabu wakati akitibiwa katika hospitali ya Mkoa Mount Meru,mbele ya chombo cha habari ,akiwa na mtoto wake mchanga,alisema kuwa juzi majira ya saa 9 alasiri mume wake alirejea nyumbani na kuuliza chakula ,hata hivyo alimjibu kuwa hakupika kwa sababu hukuacha pesa.
"Ndipo alipoanza kunipiga ngumi kichwani ,nilikimbilia nje na kuendelea kuosha vyombo na niliporejea ndani aliendelea kunipiga ngumi kichwani na mdomoni bila kujali mtoto mdogo nilie naye hadi meno yangu yakang'oka"alisema.
Mmoja ya wasamaria wema,Rosemary Masawe ambaye ni mhudumu wa afya ngazi ya jamii,katika eneo hilo ,alisema kuwa baada ya kupata taarifa za tukio hilo,alifika na kumsaidia kumpeleka hospitali ikiwa ni pamoja na kufichua tukio hilo kituo cha polisi.
Rosemary ambaye pia ni mjumbe wa serikali ya mtaa alisaidia kumtafuta mfadhili aitwaye Michael Rogati Shayo ambaye alifanikisha matibabu ya mwanamke huyo kwa kumlipia matibabu ,dawa na kuahidi kuendelea kumhudumia hadi hapo hali yake itakapotengamaa.
"Mimi kama mwanamke nimeumia sana na kitendo hiki ,nili!mua kumsaidia kumpeleka hospitali ambapo alitibiwa kwa kufungwa waya kwenye meno ila naomba polisi washughulike na matukio ya aina hii"alisema.
Shayo alikemea vikali kitendo cha ukatili kwa mwanamke kilichofanywa mume wake na kulitaka jeshi la polisi kuchukua hatua kali ili iwe fundisho kwa wanaume wengine wenye tabia kama hiyo.
Naye balozi wa eneo hilo,Joyce Abraham alisema kuwa kijana huyo amekuwa na tabia ya kumpiga mke wake mara kwa mara bila kujali mtoto mdogo aliyenaye na kudai kuwa tayari ametoa taarifa kwa jeshi la polisi na mtuhumiwa Zuberi Mbonea anatafutwa mara baada ya kutoweka baada ya tukio hilo.
Ends....
0 Comments