MKUTANO wa 44 wa shirikisho la mpira wa Miguu Afrika (CAF) unatarajiwa kutafanyika kesho Agosti 10 jijini hapa ukitarajiwa kuhudhuriwa na
mataifa 58 afrika na wageni zaidi ya 500 kutoka ndani na nje ya nchi.
mataifa 58 afrika na wageni zaidi ya 500 kutoka ndani na nje ya nchi.
Akizungumzia maandalizi ya mkutano huo, waziri wa utamaduni,sanaa na michezo, Mohamed Mchengerwa ,alisema mpaka sasa maandalizi yamekamilika kila jambo linaenda vyema kwani tayari wageni wameanza kuingia tangu tarehe 27 na wanaendela kufika hapa nchini.
Alisema mkutano huo utafunguliwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
“Tunataraji kupokea nchi 58 Kutoka bara letu la Afrika akiwemo pia Rais wa FIFA FIFA’ Gianni Infantino hivyo ugeni huu ni mkubwa sana na hili linatokea katika jiji la Arusha,”alisema waziri.
Alisema Rais wetu Samia Suluhu ameendelea kufanya makubwa katika sekta yetu ya michezo na hili ni moja ya tukio kubwa linalotokea katika kipindi hiki akiwa anaongoza serikali hii ya awamu ya sita na mengine yataendelea kutoka kwani ni jitihada kubwa na kuongeza kuwa wananchi wa Arusha watambue kuna jambo hili kubwa mkoani hapa.
Naye Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania Walace Karia ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ndani alisema ni mkutano mkuu wa mwaka wa kawaida unaofanyika kwa mara ya kwanza nchini .
Alisema nchi zote 58 zinawakiliswa ila mwaka huu nchi mbili kenya na Zimbabwe hawatashiriki kwani wamesimamsishwa na mkutano uliopita wa FIFA kutoka na masula yaliyotokea kwao..
"Mbali na nchi 58 watakuwepo waandishi wa habari kutoka mataifa mbalimbali wapatao 100 na mkutano huu unatarajiwa kutazamwa na watu zaidi ya bilioni 1 duniani kupitia vyombo vya habari"
"Pia katika mkutano huu watakuwepo wachezaji wa Zamani maarufu, Rais wa FIFA atakuwepo ambaye nae amemualika Rais wa shirikisho la soka Qatar kuwakilisha bara la Asia bila kusahau Rais wa Shirikisho la soka barani Afrika (Caf) Patrice Motsepe atakuwepo"
"Kawaida kikao hiki ni cha mwaka na kinapokea taarifa mbalimbali za utekelezaji kwa mambo ya soka kwa bara la Afrika kwa mwaka na kama kutakuwa na jambo la kisheria ama kikanuni litafanyika na taarifa zinazopokelewa ni tarifa za kawaida kwenye mikutano ikiwa ni pamoja na utekelezaji, fedha ukaguzi na kwa kipindi hiki hakuna ajenda ya uchaguzi,"alisema Karia.
Aliongeza kuwa kutakuwa na tukio litakalo fanyika la 'African super league' ambayo itazinduliwa hapa katika mkutano huu na Rais na kusema Wajumbe wasiopungua 500 watahudhuria mkutano huo.
Karia alifafanua kuwa ni fursa kubwa Tanzania imeipata kupitia mkutano huu ikizingatiwa Arusha ni kitovu cha utalii na kama Shirikisho wameamua kutumia michezo kuhamasisha utalii.
Naye Mkuu wa mkoa Arusha John Mongela alisema kama serikali wanashirikiana vyema na TFF kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa kwa wageni hawa kufika hadi kuondoka .
"Tutahakikisha Arusha inakuwa alama hivyo wanaArusha tuwe wakarimu kama inavyojulikana ukarimu wetu ili wageni watakapoondoka waende kuwa mabalozi katika kuitangaza nchi yetu,"alisema Mongela.
Ends..
0 Comments