Waziri Mkuu wa zamani wa Japan, Shinzo Abe amefariki dunia baada ya kupigwa risasi alipokuwa akihutubia kwenye kampeni za uchaguzi wa ubunge katika mji wa Nara nchini humo.
Abe (67) alipigwa risasi mara mbili ambapo moja imempata kifuani na nyingine mgongoni ambayo ilisababisha aanguke chini.
Waziri Mkuu wa sasa wa nchi hiyo, Fumio Kishida alisema hali ya Abe kuwa mtuhumiwa alikamatwa baada ya kumpiga risasi Abe.
Abe, ambaye alikuwa waziri mkuu aliyekaa muda mrefu zaidi madarakani nchini Japan, alijiuzulu mwaka 2020 akitoa sababu za kiafya.
Alirithiwa na mshirika wake wa karibu Yoshihide Suga, ambaye baadaye nafasi yake ilichukuliwa na Fumio Kishida.
0 Comments