WAZIRI MAKAMBA AZINDUA BODI MPYA,SHIRIKA LA TPDC



Waziri wa Nishati, January  Makamba amezindua bodi ya wajumbe nane wa shirika la Maendeleo ya Mafuta Tanzania(TPDC) na kuitaka bodi hiyo kuhakikisha shirika hilo linatoa mchango mkubwa katika uendelezaji wa uchumi wa mafuta na Gesi hapa nchini.

Makamba alisema kuwa uzinduzi wa bodi hiyo umetokana na Rais Samia Suluhu Hasan kumteua mwenyekiti wa bodi hiyo,Ombeni Sefue .

Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Arusha, alisema kuwa shirika la TPDC ni shirika la kimkakati lililoanzishwa mwaka 1969 kwa lengo la kuendeleza nishati ya mafuta na gesi hapa nchini.



Waziri Makamba aimeitaka bodi hiyo kusimamia shirika hilo katika utafutaji na uendelezaji wa mafuta na gesi ,ambapo Tanzania kwa sasa inazalisha gesi kuhakikisha gesi inayopatikana inauzwa nje ya nchi.

Alisema uendeshaji wa shirika hilo lazima uzingatie dira na mwelekeo wa nchi katika uchumi mpya wa gesi na uendelezaji  na utafutaji wa Mafuta Tanzania. 

Aliitaka bodi hiyo kuisaidia serikali katika kutimiza ndoto yake, kwa kuwezesha uchumi wa mafuta na gesi unachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya taifa.



"Rai yangu kwa  bodi hii ifanyekazi kwa kuisaidia serikali kutimiza ndoto ya taifa letu kwa kuwezesha uchumi wa mafuta na gesi na TPDC  kama shirika kuhakikisha linatoa mchango wake katika uendelezaji wa rasilimali watu na ushiriki wa nchi katika miradi mikubwa"alisema 

Mwenyekiti wa Bodi ya shirika la TPDC, Ombeni Sefue, amemhakikishia Waziri Makamba kuwa yeye na wajumbe wa bodi yake wako tayari kufanya kazi hiyo kwa heshima kubwa na kuhakikisha kuwa shirika hilo linatimiza malengo yake katika kuendeleza rasilimali ya mafuta na gesi hapa nchini

"Sisi kama bodi mpya tunaenda kusukuma mbele shughuli za shirika la TPDC,kuhakikisha  linatekeleza majukumu yake kwa weredi mkubwa "alisema.



Kwa upande wake mkurugenzi wa TPDC ,Dkt James Mataragio alisema ujio wa bodi hiyo utasaidia sana katika kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ili kufikia adhima ya taifa,kwani kwa muda mrefu shirika hilo limekuwa likijiendesha bila bodi.

Alisema shirika la TPDC limepewa dhamana ya kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ukiwemo mradi wa LNG(Liquefied Natural Gas) utakaogharimu zaidi ya dola za kimarekani  bil.40,mradi
 wa kutafuta mafuta mnazi bei ,mradi wa kujenga bomba la mafuta kutoka uganda kwenda Tanga na miradi ya kutafuta mafuta kutoka bonde la Ufa.

Alisema miradi hiyo itakwenda  kubabadili maisha ya watanzania kwa uanzishwaji wa viwanda  lukuki na kuwataka wananchi kuunga mkono miradi hiyo.

ends....


















Post a Comment

0 Comments