WATOTO WATANO WA FAMILIA MOJA WAFA KWA KUNYWA MAZIWA YENYE SUMU

Mkuu wa wilaya Monduli Frank Mwaisumbe 






Na Joseph Ngilisho ,Monduli

WATOTO watano wa familia moja wenye umri wa miaka 2 hadi 10 wakazi wa Mswakini chini wilayani Monduli mkoani hapa ,wamefariki dunia wakidaiwa kunywa maziwa yanayosadikiwa  kuwa na Sumu.

Akiongea na vyombo vya habari mkuu wa wilaya ya Monduli ,Fank Mwaisumbe alisema kuwa watoto hao walifariki Julai 17 mwaka huu wakati wakipatiwa matibabu katika hospitali  ya mkoa Mount Meru.

"Mmoja ya watoto hao alitangulia kufariki julai 5 mwaka huu na kuzikwa baada ya jitihada za kumpatia matibabu kushindikana ,hawa wanne wamefariki juzi wakiwa wanapatia wamelazwa mount Meru alisema 

Aliwataja marehemu hao kuwa ni ,Saimalye Nyangusi(8)Lemali Nyangusi(8)Sophia Nyangusi(8) na Veronica  Nyangusi (4) Wote wakati za Mswakimi Chini ,Makuyuni wilayani Monduli.

Hata hivyo mkuu hiyo wa wilaya alisema kuwa wazazi wa marehemu ,Nyangusi Mollel(45) na Nangoye Nyangusi(32)wanashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa uchunguzi wa tukio hilo. 

Alifafanua  kuwa chanzo cha tukio hilo ni marehemu hao kudaiwa kunywa maziwa yanayosadikiwa  kuwa na sumu ambapo baada ya kuyatumia walianza kujaa na kuvimba matumbo ndipo walipopelekwa katika kituo cha afya cha kijeshi TMA,wilayani Monduli na baadaye kuhamishiwa katika hospitali ya rufaa,Mount Meru walikofikwa na mauti.

Mmoja ya wanafamilia hiyo,Kilanian Lendoya alisema kuwa tukio lilianza mnamo.julai Mosi mwaka huu ambapo mtoto mmoja wapo Lopoi Nyangusi (6)aliugua na kupoteza hafamu na kupelekwa katika katika hospitali  moja wapo iliyopo wilayani karatu.

Alisema siku ya tano,Julai 5 mwaka huu akiwa amelazwa katika  hospitali hiyo alifariki dunia na kuzikwa nyumbani kwao Mswakini. 

Alisema alisema kuwa baba yao Nyangusi  Mollel mwenye watoto saba,watoto wengine wanne waliendelea kuumwa na ilipofika julai 16 walipelekwa katika kituo cha afya cha jeshi la wananchi Tanzania TMA Monduli .

Alisema kuwa Julai 17 walitolewa hospitalini kwa ajili ya kupelekwa maombi kuombewa kutokana na ugonjwa wanaoumwa kutojulikana , lakini ghafla hali zao zilibadilika na kupelekwa katika hospitali ya mkoa Mount Meru ambapo walifariki dunia kwa kupokezana.

Miili ya merehemu imehifadhiwa katika chumba cha maiti katika hopitali ya mkoa Mount Meru kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Ends...









Post a Comment

0 Comments