Na Joseph Ngilisho, Manyara.
WAREMBO nane kati ya 50 mashuhuri duniani wanaoshiriki shindano la Miss Jungle international 2022 wametembelea mgodi wa madini ya Tanzanite ambao Rais Samia Sulubu alishiriki kutengeneza filamu ya Royal tour .
Mgodi huo wa kampuni ya Franone Mining, umepata umaarufu wa aina yake , baada ya
warembo hao kuwa na shauku ya kuingia ndani ya mgodi huo kujionea uzalishaji wa madini pekee adimu duniani ili kuitangaza Tanzania na vivutio vyake .
Mmoja ya waandaaji wa shindano hilo,Martin Rajabu alisema ziara hiyo imekuja baada ya warembo hao kuiona filamu ya Royal Tour na kuhamasika kuja nchini kujionea vivutio hivyo ,hususani yanapopatikana madini adimu duniani ya Tanzanite .
Adha alisema kuwa warembo hao pia watatembelea vivutio vyote ambavyo rais Samia alivionyesha katika Filamu ya Royal Tour na wameahidi kuwa mabalozi wazuri wa kuitangaza Tanzania kimataifa baada ya kujionea vivutio hivyo .
"Baada ya ziara hii ya kutembelea madini ya Tanzanite Mererani, watakwenda pia kwenye mbunga za wanyama ,Ngorongoro, Tarangile,Serengeti na Kizimkazi Zanzibar ambako ndiko makazi ya Rais Samia na chimbiko la Royal Tour "alisema.
Warembo hao licha ya kuingia mgodini na kuona madini hayo yanavyochimbwa katika mgodi wa kampuni ya Franone Mining ,pia walijionea jinsi madini hayo yanavyokatwa na kuthaminishwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Franone Mining, Vitus Ndakize,alisema ujio wa warembo hao mashuhuri duniani ni fursa ya kipekee kwwntu watanzania kuyatangaza madini ya Tanzanite duniani,ambayo ni madini pekee adimu dunia.
Alisema tangu Rais Samia afike katika mgodi wao wakati akirekodi Filamu ya Royal Tour, bei ya madini ya Tanzanite imeongezeka baada ya wà nunuzi mbalimbali wa kimataifa kumiminika nchini.
"Tumefurahi sana kutembelewa na warembo hao kutoka mataifa mbalimbali Dunia, kwani ni fursa ya kipekee kwenye kuitangaza Tanzanite na kuitangaza Tanzania na vivutio vyake ,rais Samia baada ya kutembelea mgodi wetu tumeona bei ya Tanzanite imebadilika na wanunuzi wameongezeka "alisema
Akiongea mmoja ya warembo hao ,Zulema Vazquez Rey )Miss Europe Spain)alisema amefurahi kufika Nchini Tanzania na kujionea madini ya Tanzanite ambayo ni madini pekee duniani yanayo patikana Tanzania na wanatarajia kujionea vivutio vingine mbalimbali ikiwa ni njia pekee ya kuitangaza Tanzania na vivutio vyake.
"Kwakweli nimefarijika sana kufika Tanzania na nimeweza kuona namna madini haya ya Tanzanite yanavyo chimbwa,kupimwa hadi kufikishwa sokoni duniani kote, kwakweli madini haya ni pekee duniani na leo nafarijika kufika katika mgodi huu wa Flanone Mining na kuona uchimbaji ni wakisasa na ninaamini nitakuwa balozi mzuri wa madini haya". Alisema Miss Zulema Vazquez Rey.
Kwa upande wake Miss Jangle kutoka Tanzania, Dorine Gibson Mwapongo, alisema juhudi anazo fanya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan za kutangaza vivutio vya utalii pamoja na madini ya Tanzanite inapaswa kuungwa mkono kwa juhudi zote na wao kama warembo kupitia mashindano ya Miss Jungle ambapo wamepanga kuitangaza Tanzanite ulimwenguni kote.
"Tumepata nafasi ya kutembelea mgodi wa flanone hapa mererani ni fahari kubwa sana kwetu na tumeweza kujifunza vitu vingi sana juu ya madini lakini pia tutatembelea sehem zete ambazo Rais alitembelea ili kujifunza zaidi na kuhakikisha tunaitangaza Tanzania kwa moyo mmoja na uzalendo wa taifa letu". Alisema Miss Dorine.
Ends..
0 Comments