Na Joseph Ngilisho Arusha
Marais wa nchi 7 wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wanatarajia kukutana jijini Arusha(Leo) kesho Julai 21 na 22, 2022 katika kujadiliana juu ya maendeleo ya jumuiya hiyo ikiwemo kupitisha lugha ya kiswahili kutumika rasimi ndani ya jumuiya hiyo.
Akiongea na vyombo vya habari ,katibu Mkuu wa EAC, Dk Peter Mathuki akizungumza alisema, kikao hicho kitakuwa na umuhimu kwani marais wataweza kuangalia namna jumuiya inavyoendelea na kujadili changamoto zilizopo.
Alisema wakuu wa nchi wanaotarajiwa kuhudhuliwa kikao hicho ni Samia Suluhu Hassan (Tanzania), Paul Kagame (Rwanda), Uhuru Kenyatta (Kenya), Yoweri Mseven (Uganda), Evariste Ndayishimiye (Burundi) Félix Tshisekedi (DR Congo) na Salva Kiir (Sudan kusini).
"Wataangalia jumuiya inavyoendelea, changamoto gani na kusukuma maendeleo ya jumuiya ili wananchi wa jumuiya hiyo waendele kufaidika," alisema
Dk Muthuki alisema marais hao pia watazindua barabara ya mchepuo ya Afrika ya Mashariki iliyojengwa na Serikali kwa kushirikiana na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
"Watazindua barabara ya East African Bypus na baadae watakuwa na kikao rasmi wakuu wa Marais," alisema
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella alisema mandalizi yapo vizuri kwa kushirikiana na sekretalieti ya EAC inayoundwa na nchi saba.
Naye waziri wa Mambo ya Nje ,balozi Liberata Mulamula alisema kikao hicho kitatanguliwa na kikao cha mawaziri wa EAC kitakachoangazia changamoto na ustawi wa jumuiya hiyo ikiwemo manufaa ya soko la pamoja na kutoa maadhimio na mapendekezo .
"Tutajadili masuala mbalimbali yanayohusu mtangamano wa jumuiya, pamoja na soko la pamoja katika kipindi cha miaka 11 tumetoka wapi tuko wapi na tunaendaje mbele na baadaye mapendekezo tunayapeleke katika kikao cha wakuu wa nchi"alisema.
Alisema wakuu wa nchi pia watajadili na kupitisha lugha ya kiswahili na kifaransa kuwa lugha rasimi itakayotumika katika jumuiya hiyo .
"Tunafarijika kuona lugha ya kiswahili ikiingia katika umoja wa mataifa na hivyo kupitia kikao hiki wakuu wa nchi watapitisha ili lugha hiyo iwe rasmi kutumika ndani ya EAC.
Ends.....
0 Comments